Jacinta Ngobese-Zuma: Kutoka kuwa mtangazaji wa radio hadi kuongoza "March and March"

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
HLlmIKXWcAAQiJt.png

Hali sio shwari kwa wahamiaji nchini Afrika Kusini hasa wale wanaotoka mataifa ya Afrika. Maelfu ya wananchi kutoka Nigeria, Ghana, Malawi, Zimbabwe na Zambia na nyinginezo, wanatakiwa waondoke nchini humo kabla ya Juni 30, 2026.

Siku hiyo yamepangwa maandamano makubwa ya kuwafukuza wahamiaji wanaodaiwa kutokuwa na nyaraka za uhamiaji. Maandamano hayo yamepangwa na vuguvugu la March and March linaloongozwa Jacinta Ngobese-Zuma.

Jacinta ni nani?

Ni mwanahabari wa Afrika Kusini na mwanaharakati mashuhuri anayepinga uhamiaji, anayeishi mjini Durban.

Kabla ya kujikita kikamilifu katika uanaharakati, Ngobese-Zuma alikuwa mtangazaji maarufu wa redio katika Vuma FM mjini Durban, ambapo alijijengea hadhira kubwa katika eneo la KwaZulu-Natal. Baada ya mkataba wake wa utangazaji kutoongozwa mwaka 2025, alielekeza nguvu zake katika uanaharakati wa kijamii unaotumia mitandao ya kijamii na kampeni za wananchi.

Utaalamu wake katika uandishi wa habari umekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya harakati zake. Wachambuzi na wakosoaji wanaeleza kuwa matumizi yake ya mitandao ya kijamii kama TikTok, ujumbe wenye hisia kali na mawasiliano ya moja kwa moja na umma yameisaidia harakati yake kukua haraka kutoka ngazi ya eneo moja hadi kampeni inayofanyika katika majimbo mbalimbali ya Afrika Kusini.

Harakati za “March & March”​

Ngobese-Zuma alianzisha harakati za March & March kama jukwaa la wananchi linalotetea mageuzi ya sera za uhamiaji nchini Afrika Kusini.

Harakati hiyo huandaa maandamano, mikutano na waandishi wa habari na mikusanyiko mbalimbali inayolenga kile wanachokieleza kuwa athari za kijamii na kiuchumi za uhamiaji.

Miongoni mwa madai makuu ya harakati hiyo ni kutaka udhibiti mkali zaidi wa mipaka na utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo za uhamiaji, kutaka kusitishwa kwa mchakato wa kushughulikia maombi ya wakimbizi na kuhamishwa kwa wingi kwa raia wa kigeni wasiokuwa na nyaraka halali, utanguliza raia wa Afrika Kusini katika ajira, huduma za afya, elimu na fursa za biashara ndogondogo.
snzgwW7z.jpg

Mtazamo wa Kisiasa na Simulizi Binafsi​

Ngobese-Zuma mara nyingi hutumia simulizi za maisha yake binafsi kujenga mvuto wa kisiasa. Katika video mbalimbali zilizosambazwa sana mtandaoni, ameeleza uzoefu wa utotoni uliomhusisha mama yake na raia wa kigeni kama sehemu ya sababu zinazomfanya kuzingatia masuala ya udanganyifu wa uhamiaji na kuwa na mtazamo mkali kuhusu wahamiaji.

Ingawa yeye na harakati yake wanasisitiza kuwa kampeni zao zinahusu uwajibikaji wa kisheria na suala la wahamiaji wasio na nyaraka, wakosoaji, mashirika ya haki za binadamu na wachambuzi wa siasa wanasema kauli zake za kisiasa zinaweza kuchochea chuki dhidi ya wageni (xenophobia).

Wanaonya kuwa mara nyingi kampeni hizo huchanganya wahamiaji haramu, wahamiaji halali na wakimbizi, jambo linaloweza kuongeza hisia za kupinga wageni katika miji mikubwa ya Afrika Kusini pamoja na harakati zinazohusishwa na wanaharakati wengine kama Zandile Dabula.
4h4R9VsiM_8Adk3p.jpg

Kesi za Kisheria​

Mwanzoni mwa mwaka 2026, mashtaka ya kuchochea vurugu yaliwasilishwa kufuatia maandamano ya harakati za March & March nje ya shule ya msingi mjini Durban. Ngobese-Zuma alijisalimisha mwenyewe kwa vyombo vya sheria ili kushughulikia tuhuma hizo.

Mjadala Kuhusu Matumizi ya Fedha za Serikali​

Katikati ya mwaka 2026, Ngobese-Zuma alikosoa hadharani uamuzi wa serikali ya Afrika Kusini wa kutenga zaidi ya rand milioni 600 kwa ajili ya shughuli za ulinzi na usimamizi wa usalama wa umma kabla ya maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika Juni 30.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, ikiwemo SABC, alisema kuwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaonyesha kuwa serikali tayari ina uwezo wa kifedha na rasilimali watu za kutosha kulinda mipaka na kukabiliana moja kwa moja na uhamiaji haramu.

Harakati yake pia imevutia mjadala wa kitaifa kwa kuandaa maandamano dhidi ya matukio ya kiutamaduni yenye utata, ikiwemo sherehe ya kutawazwa kwa mtu aliyejitangaza kuwa mfalme wa Waigbo katika Eastern Cape, tukio lililozua mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya wageni na utambulisho wa kitaifa nchini Afrika Kusini.

Vuguvugu la wahamiaji linavyotishia ANC uchaguzi ujao
Ramaphosa.png

Kuibuka kwa harakati zenye nguvu za kupinga uhamiaji kama March & March na Operation Dudula kumeiweka chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), katika moja ya nyakati zake ngumu zaidi kisiasa tangu kuingia madarakani mwaka 1994.

Wakati Afrika Kusini ikielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Novemba 2026, mamlaka ya ANC, rekodi yake ya utawala na msingi wake wa jadi wa wapiga kura vinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuongezeka kwa siasa za kizalendo kali na hisia za kupinga wahamiaji.

Udhaifu mkubwa wa ANC unatokana na ukweli kwamba harakati za kupinga uhamiaji zinatumia malalamiko yale yale ambayo serikali imeshindwa kuyatatua kwa miaka mingi. Miongoni mwa changamoto hizo ni kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira, kuzorota kwa huduma za umma na ongezeko la pengo la kiuchumi kati ya matajiri na maskini.

Makundi kama March & March yamekuwa yakielekeza lawama kwa wahamiaji wa kigeni kwa matatizo hayo. Kwa kuwa ANC imekuwa ikishindwa kutoa suluhisho la haraka kwa changamoto za kiuchumi, imeanza kupoteza ushawishi wake katika maeneo ya wafanyakazi na vitongoji vya watu wa kipato cha chini.

Vyama vya siasa vinavyotumia hoja za kizalendo, hasa uMkhonto weSizwe Party (MK Party) kinachoongozwa na Jacob Zuma, vimekuwa vikichukua au kuunga mkono sehemu ya ujumbe wa harakati hizo ili kuvutia wapiga kura ambao kwa muda mrefu walikuwa ngome ya ANC.

Mabadiliko ya Sera na Lugha ya Kisiasa

Katika jitihada za kuendelea kuwa na mvuto wa kisiasa, ANC imelazimika kubadilisha msimamo wake na kuonyesha ukali zaidi kuhusu masuala ya uhamiaji.

Serikali ya Rais Cyril Ramaphosa imeongeza ahadi za kuimarisha ukaguzi wa maeneo ya kazi na kuwaadhibu waajiri wanaowaajiri wahamiaji wasio na nyaraka kwa mishahara midogo, kuimarisha ulinzi wa mipaka na kufanya marekebisho ya sheria za uhamiaji, kupambana na rushwa ndani ya Department of Home Affairs.

Ingawa Ramaphosa amesisitiza mara kadhaa kuwa uhamiaji haramu si chanzo pekee cha matatizo ya uchumi wa Afrika Kusini, hatua za serikali zinaonyesha wazi kuwa ANC inalazimika kujibu shinikizo linalotokana na makundi ya kupinga uhamiaji.
 
Sasa S. Afrika ilikuwaje taifa lililoimbwa kama taifa mashuheri pengine kuliko yote Afrika likashindwa kudhibiti uhamiaji haramu! Naona taifa lao linazidi kudidimia vibaya miaka kadhaa ijayo patakuwa hapaeleweki tena huko.
 
Makundi kama March & March yamekuwa yakielekeza lawama kwa wahamiaji wa kigeni kwa matatizo hayo
Wasauzi hawajitambui. Wazungu wana miliki 73% ya ardhi yote ya kilimo Afrika kusini na wamekamata uchumi kwa zaidi ya 80% cha ajabu wao hawana shida na Wazungu in fact walikipa kura za kutosha hadi kukiweka chama hiko kuwa serikalini. Na kwa kura za maoni za mwezi huu chama cha makaburu ndio kinaungwa mkono zaidi Afrika kusini.

Huwa nashindwa kuelewa wanataka nini hasa.
 
Kuongezea, whites Afrikaans make about only 7.2% of the total population of 63m. Na wana hold 73% ya land, uchumi wana hold more than 80%! Cha ajabu mi afrika yenzetu inatubaguwa sisi weusi wenzao! Kututisha, katunyanyasa, kututesa na hata kutuuwa!
Tujaribu kujuuliza, wale weusi wa huko wasiotupenda na kutuchukia wahamiaji wa kiafrika wana AKILI za namna gani?!?!
Wamesahau jinsi tulivyowapenda, kuwapa hifadhi, kutumia passport zetu na hata kuwachangia fedha na jasho letu!
Pale morogoro mazimbo mbona hatukulalamika walivyokuwa wanatembea na dada au mama zetu?!
Nataka kutoa tusi lakini nadhani halitasaidia hii thread...
 
View attachment 3615396
Hali sio shwari kwa wahamiaji nchini Afrika Kusini hasa wale wanaotoka mataifa ya Afrika. Maelfu ya wananchi kutoka Nigeria, Ghana, Malawi, Zimbabwe na Zambia na nyinginezo, wanatakiwa waondoke nchini humo kabla ya Juni 30, 2026.

Siku hiyo yamepangwa maandamano makubwa ya kuwafukuza wahamiaji wanaodaiwa kutokuwa na nyaraka za uhamiaji. Maandamano hayo yamepangwa na vuguvugu la March and March linaloongozwa Jacinta Ngobese-Zuma.

Jacinta ni nani?

Ni mwanahabari wa Afrika Kusini na mwanaharakati mashuhuri anayepinga uhamiaji, anayeishi mjini Durban.

Kabla ya kujikita kikamilifu katika uanaharakati, Ngobese-Zuma alikuwa mtangazaji maarufu wa redio katika Vuma FM mjini Durban, ambapo alijijengea hadhira kubwa katika eneo la KwaZulu-Natal. Baada ya mkataba wake wa utangazaji kutoongozwa mwaka 2025, alielekeza nguvu zake katika uanaharakati wa kijamii unaotumia mitandao ya kijamii na kampeni za wananchi.

Utaalamu wake katika uandishi wa habari umekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya harakati zake. Wachambuzi na wakosoaji wanaeleza kuwa matumizi yake ya mitandao ya kijamii kama TikTok, ujumbe wenye hisia kali na mawasiliano ya moja kwa moja na umma yameisaidia harakati yake kukua haraka kutoka ngazi ya eneo moja hadi kampeni inayofanyika katika majimbo mbalimbali ya Afrika Kusini.

Harakati za “March & March”​

Ngobese-Zuma alianzisha harakati za March & March kama jukwaa la wananchi linalotetea mageuzi ya sera za uhamiaji nchini Afrika Kusini.

Harakati hiyo huandaa maandamano, mikutano na waandishi wa habari na mikusanyiko mbalimbali inayolenga kile wanachokieleza kuwa athari za kijamii na kiuchumi za uhamiaji.

Miongoni mwa madai makuu ya harakati hiyo ni kutaka udhibiti mkali zaidi wa mipaka na utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo za uhamiaji, kutaka kusitishwa kwa mchakato wa kushughulikia maombi ya wakimbizi na kuhamishwa kwa wingi kwa raia wa kigeni wasiokuwa na nyaraka halali, utanguliza raia wa Afrika Kusini katika ajira, huduma za afya, elimu na fursa za biashara ndogondogo.
View attachment 3615398

Mtazamo wa Kisiasa na Simulizi Binafsi​

Ngobese-Zuma mara nyingi hutumia simulizi za maisha yake binafsi kujenga mvuto wa kisiasa. Katika video mbalimbali zilizosambazwa sana mtandaoni, ameeleza uzoefu wa utotoni uliomhusisha mama yake na raia wa kigeni kama sehemu ya sababu zinazomfanya kuzingatia masuala ya udanganyifu wa uhamiaji na kuwa na mtazamo mkali kuhusu wahamiaji.

Ingawa yeye na harakati yake wanasisitiza kuwa kampeni zao zinahusu uwajibikaji wa kisheria na suala la wahamiaji wasio na nyaraka, wakosoaji, mashirika ya haki za binadamu na wachambuzi wa siasa wanasema kauli zake za kisiasa zinaweza kuchochea chuki dhidi ya wageni (xenophobia).

Wanaonya kuwa mara nyingi kampeni hizo huchanganya wahamiaji haramu, wahamiaji halali na wakimbizi, jambo linaloweza kuongeza hisia za kupinga wageni katika miji mikubwa ya Afrika Kusini pamoja na harakati zinazohusishwa na wanaharakati wengine kama Zandile Dabula.
View attachment 3615399

Kesi za Kisheria​

Mwanzoni mwa mwaka 2026, mashtaka ya kuchochea vurugu yaliwasilishwa kufuatia maandamano ya harakati za March & March nje ya shule ya msingi mjini Durban. Ngobese-Zuma alijisalimisha mwenyewe kwa vyombo vya sheria ili kushughulikia tuhuma hizo.

Mjadala Kuhusu Matumizi ya Fedha za Serikali​

Katikati ya mwaka 2026, Ngobese-Zuma alikosoa hadharani uamuzi wa serikali ya Afrika Kusini wa kutenga zaidi ya rand milioni 600 kwa ajili ya shughuli za ulinzi na usimamizi wa usalama wa umma kabla ya maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika Juni 30.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, ikiwemo SABC, alisema kuwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaonyesha kuwa serikali tayari ina uwezo wa kifedha na rasilimali watu za kutosha kulinda mipaka na kukabiliana moja kwa moja na uhamiaji haramu.

Harakati yake pia imevutia mjadala wa kitaifa kwa kuandaa maandamano dhidi ya matukio ya kiutamaduni yenye utata, ikiwemo sherehe ya kutawazwa kwa mtu aliyejitangaza kuwa mfalme wa Waigbo katika Eastern Cape, tukio lililozua mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya wageni na utambulisho wa kitaifa nchini Afrika Kusini.

Vuguvugu la wahamiaji linavyotishia ANC uchaguzi ujao
View attachment 3615402
Kuibuka kwa harakati zenye nguvu za kupinga uhamiaji kama March & March na Operation Dudula kumeiweka chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), katika moja ya nyakati zake ngumu zaidi kisiasa tangu kuingia madarakani mwaka 1994.

Wakati Afrika Kusini ikielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Novemba 2026, mamlaka ya ANC, rekodi yake ya utawala na msingi wake wa jadi wa wapiga kura vinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuongezeka kwa siasa za kizalendo kali na hisia za kupinga wahamiaji.

Udhaifu mkubwa wa ANC unatokana na ukweli kwamba harakati za kupinga uhamiaji zinatumia malalamiko yale yale ambayo serikali imeshindwa kuyatatua kwa miaka mingi. Miongoni mwa changamoto hizo ni kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira, kuzorota kwa huduma za umma na ongezeko la pengo la kiuchumi kati ya matajiri na maskini.

Makundi kama March & March yamekuwa yakielekeza lawama kwa wahamiaji wa kigeni kwa matatizo hayo. Kwa kuwa ANC imekuwa ikishindwa kutoa suluhisho la haraka kwa changamoto za kiuchumi, imeanza kupoteza ushawishi wake katika maeneo ya wafanyakazi na vitongoji vya watu wa kipato cha chini.

Vyama vya siasa vinavyotumia hoja za kizalendo, hasa uMkhonto weSizwe Party (MK Party) kinachoongozwa na Jacob Zuma, vimekuwa vikichukua au kuunga mkono sehemu ya ujumbe wa harakati hizo ili kuvutia wapiga kura ambao kwa muda mrefu walikuwa ngome ya ANC.

Mabadiliko ya Sera na Lugha ya Kisiasa

Katika jitihada za kuendelea kuwa na mvuto wa kisiasa, ANC imelazimika kubadilisha msimamo wake na kuonyesha ukali zaidi kuhusu masuala ya uhamiaji.

Serikali ya Rais Cyril Ramaphosa imeongeza ahadi za kuimarisha ukaguzi wa maeneo ya kazi na kuwaadhibu waajiri wanaowaajiri wahamiaji wasio na nyaraka kwa mishahara midogo, kuimarisha ulinzi wa mipaka na kufanya marekebisho ya sheria za uhamiaji, kupambana na rushwa ndani ya Department of Home Affairs.

Ingawa Ramaphosa amesisitiza mara kadhaa kuwa uhamiaji haramu si chanzo pekee cha matatizo ya uchumi wa Afrika Kusini, hatua za serikali zinaonyesha wazi kuwa ANC inalazimika kujibu shinikizo linalotokana na makundi ya kupinga uhamiaji.

Anastahili pongezi yeye na wana vugugugu wenzie kwa kudai mabadiliko
 
Back
Top Bottom