Jack Patrick kutupwa JELA miaka 10..!!

Jack Patrick kutupwa JELA miaka 10..!!

Duh! Habari mpya kutoka huko Hong Kong, China zinaeleza kuwa kama atapatikana na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ atatumikia kifungo cha miaka kumi jela.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikwenda kumtembelea Jack akiwa nyuma ya nondo baada ya kuruhusiwa kumuona tangu Machi mosi, mwaka huu, mwanamitindo huyo amekata tamaa na hana matumaini ya kutoka jela hivi karibuni.

“Aisee Jack Cliff anatia huruma sana, hana matumaini ya kutoka hivi karibuni na ana maumivu ya kupitiliza,” kilisema chanzo hicho.
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Jack anasema kuwa kesi yake ni ngumu na endapo atapatikana na hatia, basi atakumbana na kifungo, si chini ya miaka kumi, jambo ambalo limemfanya kudondosha machozi kila kukicha huku akituma salamu nyumbani kwao Bongo.



Jack alikamatwa na unga kilo 1.1 huko Macau, Hong Kong mwezi Desemba, mwaka jana ambapo sasa kesi yake itaanza kuunguruma Septemba, mwaka huu.
Macau ipo Hongkong? kama kitu hujui ni bora kuuliza.
 
Kumbe anabahati. Miaka Kami tu? Nilifikiri wanakata shingo.

Angeshikwa china bara angenyongwa ila ameshikwa visiwani kwenye jimbo ambalo lilijitenga na sheria za china
 
Hivi, haruhusiwi kumtaja aliyemtuma? Kama atafungwa, huyo boss wa madawa atarecruit vijana wengine au sio?Vijana wataendelea kuangamia mpaka lini?

Tatizo ni ushahidi pia uyo hamjui boss wake anawajua ma agent wa boss tu
 
Akome!laiti hawa punda wangejua madhara wanayowasababishia vijana wetu wabwia unga,nadhani wangeacha kusafirisha haya makitu!
 
akikutwana na hatia apigwe hata miaka 50 fresh tu,we have to learn kwamba no shortcut in life.
 
Nimepata huzuni ghafla kwa ajili yake..so sorry for her..she s too beautiful for that...
 
hivi mabosslady huwa wanalipa kodi kutokana na shughuli zao?
 
Hapana Dinazarde, Tiff alipata dhamana baada ya kukaa ndani takribani mwala mzima,yuko mtaani toka May 2013.

Afadhali kama alitoka maana alimpa kila kitu huyo bossushuz lakin alivyokamatwaa akawekwa jela huyu Jack ndio ikawa furaha kwake!! najua atafight atapata pesa tu,
 
hehehehe haya naomba ajitokeze hapa yule anaetetea mashangingi ya mjini wajasiriamali na wanaenda kuchukua mizigo China :biggrin1:
 
Back
Top Bottom