TANZIA Jackson Makwetta (Mbunge na Waziri wa zamani) afariki dunia

mkuuu wa nchi sijui kama atakwenda kutowa salamu za rambi rambi atadai amechoka na safari ya dodoma anaitaji kupumzika

MUNGU akurehemu upumzike kwa amani
 

Mkuu hapo kwenye Red sidhani kama unaongea sawa! Jee, mazishi ya Mwalimu Nyerere hayakupewa uzito unaostahili? jee, vipi mazishi ya Sokoine, Kawawa, Mzee Rupia, Bibi Titi, nk? jee, hawa viongozi hawakuwa Wazalendo? kama jibu lako ni ndio basi utakuwa Mtanzania wa kwanza kuwatuhumu viongozi hawa kwa utovu wa uzalendo!

Vinginevyo nakuomba ukanushe kauli yako na kuwaomba msamaha familia ya wazalendo hawa!
 
rip
Haya wanasiasa wakaoshe sura na kurusha mapicha kwenye blogi ya michuzi
 
Ninamkumbuka sana makweta, tulikuwa tukimuimba katika nyimbo madarasani mwetu wakati nilipokuwa shule ya msingi miaka ya 1983 na 1984 enzi hizo akiwa ni waziri wa Elimu. Kwa kweli tulikuwa na viongozi wazalendo enzi zile, watu kama akina Rashid Mfaume Kawawa, Edward Moringe Sokoine n.K. Leo viongozi waliosalia ni balaa tupu, tumbo mbele uzalendo nyuma.
 
Mwadilifu namba moja ktk serikali alizozitumikia!

Maisha yake hafifu baada ya kustaafu yametufundisha kuwa labda inabidi uwe fisadi angalau kidogo ili usiadhirike ukistaafu kwani pensheni kiduchu wanayolipwa wastaafu ya kila mwezi haikusaidii lolote kwa hii inflation kubwa tuliyo nayo!

RIP Mzee Makweta na serikali iwaangalie sasa watumishi wake kwa kubadili pensheni zao!
 
Namkumbuka haswa enzi nikiwa shule ya msingi enzi ile Mwalimu naye alikuwa na wasifu serikalini na hata awamu ya pili ya Mwinyi alikuweko tu madarakani.

Rest In Peace Jackson Makwetta! Bwana atakufufua siku ya ufufuo! Aaamen!
 
Utashangaa msiba wa Kanumba serikali ya CCM very budy, lakini wazalendo kama Makweta hamna kitu. RIP Makweta
 
mwenyezi MUNGU amlaze pema mzee makweta na pia awajalie moyo wa uvumilivu ndugu na jamaa wote hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mtu mashuhuri
 

Kwa wanaonielewa wamenielewa; unafiki wa viongozi wetu kwenye misiba kama hii upo pale pale ndugu yangu; Na sitabadilisha kauli yangu;
 
Pamoja na kuwa na mawaziri kibao wa elimu kama akina Mayagila, Mgonja, Kapuya, Mungai n.k, marehemu Makweta ni bora kuliko wote. Namkumbuka sana kwa kuanzisha mtihani wa kidato cha pili.

Poleni sana wafiwa, RIP Makweta, J.
 
ni miongoni mwa wazee wakongwe kabisa ndani ya 'chama changu'!.....ambao kiukweli hichi 'chama changu'(mimi,fmes na pasco) kitakumbuka mchango wake mkubwa katika kukijengea sifa kubwa 'chama changu'

pumzika babu yangu!.......

you are in a better place now
 
R. I. P Makweta umelitumikia taifa lakini mchango wako haujatambulika mpaka wameshindwa kukupeleka lndia.

Siku ikifika utakufa tu hata ukienda India haisaidii.
 
Pumzika baba Makwetta umelifanyia mengi Taifa hili.RIP Makwetta.
 
Pumzika baba Makwetta umelifanyia mengi Taifa hili.RIP Makwetta Taifa linakulilia.
 
Pole sana dada Tumwa! Baba katutoka! Mungu kampenda zaidi, mungu atawafariji wakati huu mgumu wa majonzi, bwana ametoa bwana ametwaa! RIP Makweta
 
Kila nafsi itaonja mauti. Rest in peace makwetta may god rest your soul in eternally piece
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…