Jibu langu ni kwamba CCM ya sasa haina utamaduni wa kuwaenzi viongozi ambao walikuwa ni waadilifu; mifano ipo mingi, na inatakuwa ulitambue hilo badala ya kuja na mifano ya sokoine, nyerere na kawawa; natamani ningeelezea jinsi gani Mzee Makweta, licha ya kuwa muaminifu, mwadilifu na mzalendo kwa nchi yake ameteseka sana kutokana na kutekelezwa katika kipindi chote cha ustaafu wake hadi uhai wake ulipochukuliwa na Mola; Haina maana kwamba ni jukumu la chama na serikali kutunza kila kiongozi, bali kuna mengine ya aibu ambayo sina haja ya kuyajadili; Na sio yeye tu, orodha ni ndefu na mifano hai ni mingi; naomba niliachie hili suala hapa, na tukubaliane tu kutokubaliana, vinginevyo ningependa kurudia tena - sitabadilisha kauli yangu ya awali;