Mzee huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wa CCM waliotumikia taifa lao kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu, akiwa waziri wa serikali kwa miaka 25 mfululizo (1975 - 2000), lakini hakuna mahali alitumia vibaya madaraka yake kwani inasemekana kwamba hata nyumba ya kuishi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam alijengewa na wanae kabla ya kustaafu na hata hivyo haikukamilika ipasavyo; na katika kipindi karibia chote cha ustaafu wake alikuwa anaishi kwao kijijini;
Lakini kwa vile serikali yetu ya CCM haijali watu kama hawa, msiba wake utaendeshwa kinafiki tu; Misiba yenye kupewa uzito ni ile ya viongozi wasiokuwa wazalendo ambao utashi wao unapimwa kwa utajiri wao; Lakini ipo siku yote haya yatabadilika;
Poleni wafiwa; Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu Makweta, Amen;