Ni hivi baada ya kifo cha Mzee Rrginald Mengi, Benjamin Mengi, William Mushi, Zoeb Hassuji na Sylivia Novatus Mushi walifungua shauri la mirathi katika Mahakama Kuu, wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi ya Marehemu Mzee R Mengi. Baada ya hapo Shauri hilo lilitangazwa kwa umma kupitia Gazeti la Daily news na Tangazo la Serikali, ili kama kuna mtu analo pingamizi juu ya suala hilo awasilishe pingamizi ndani ya siku 30 kama Sheria inavyotaka. Watoto wawili wakubwa wa mzee Mengi waliweza kuwasilisha pingamizi ndani ya muda kupinga watajwa hapo juu kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi, hata hivyo kabla ya kuendelea kusikilizwa kwa maombi ya pingamizi husika, Jackline Mengi yeye pamoja na Watoto wake waliwasilisha maombi Mahakamani kuomba kuwasilisha na wao pingamizi la watajwa awali hapo juu kuwa wasimamizi wa mirathi nje ya muda. Kabla ya kuendelea na shauri watoto wakubwa wa mzee Mengi waliweka pingamizi la kusikilizwa kwa maombi ya Jackline kwa sababu katika kiapo chake imeonekana ameweka maelezo ya kuambiwa, maelezo yenye majumuisho n.k kitu ambacho ni kinyume na Sheria. Mheshimiwa Jaji Mlyambina amekubaliana na mapingamizi ya watoto wakubwa wa Mengi kwamba ni kweli maelezo yaliyomo katika kiapo cha Jack ni ya kusikia au kuambiwa badala ya kutoa maelezo yake yeye kama yeye maana kiapo ni ushahidi. Hivyo Mheshimiwa Jaji kaamua kuondoa maombi ya Jack Mahakamani na kila upande imeamuliwa ubebe gharama