Ujue hakutumia akili tu! Alijua fika kabisa kuwa hata akiachiwa hicho cha Mzee chote kwa maisha aliyoishi na ndugu wa Mengi ni ngumu sana yeye kuwa na nguvu ktk uendeshaji wa zile biashara,kama hawa watoto wawili wana 75% tayari,anadhani hiyo 25% anayotaka kuwatapeli pia atakuwa na maamuzi gani ktk Makampuni,kama siyo kuishia kuwa frustrated tu,ningekuwa Mimi ningekaa na kina Regina vizuri nikabaki kuwa Mpenzi mtazamaji nikisubiri mgawo wangu,wale wasingemnyima! But kwa ujuaji huu alioufanya,anakwenda kupoteza kila kitu,ashukuru kuna wale Mapacha watamfanya aishi kupitia wao!
Pia pana kitu hakukitarajia,kwamba Watu walio wengi wamemuona yeye ni Mwizi,laghai na tapeli mkubwa! The same feelings goes to hata wale wanaoisikiliza kesi yake,image yake imeharibika sana,atahitaji nguvu ya ziada kuweza kuaminika tena hasa kwenye familia ya Mengi,vinginevyo wale watoto wanakuja kuwa Wahanga wa ujuaji wa Mama yao! Mtaka yote kwa pupa hukosa yote!