Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kwa nini asitoe hoja maghorofa yajengwe kwake Kisarawe watu wahamie huko??Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni kama Buguruni, Vingunguti, Tandale na maeneo mengine ili kujenga maghorofa na kuupa hadhi Mkoa wa Dar es Salaam.
View attachment 3539631
Ana hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etcMbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.
Miaka 20 Baadaye kama bado watakuwepo watakuja kusema hayo maeneo nayo yabomolewe yajengwe maghorofa.Ana hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela
Hata ukosefu wa mipango miji ni matatizo ya msingi ya nchi yaliyosababishwa na CCMHuwa nashindwa kuelewa hawa wanasiasa kama kweli wanajua wanachokifanya. Badala ya kudili na matatizo ya msingi kabisa ya wananchi, wao wanakimbilia kufanya vitu kwa kuwaringishia wageni. Shida ya maji na umeme tu bado inatusumbua taifa zima halafu tunaongelea kupendezesha jiji sijui kwa faida ya nani. Eti huyu naye walikuwa wanampa nafasi ya kuwa rais wa nchi
Hapo ndo utajua kwa nini africa tunaitwa nyaniMiaka 20 Baadaye kama bado watakuwepo watakuja kusema hayo maeneo nayo yabomolewe yajengwe maghorofa.
Mifuko yao bado imejaa maokoto ya uchaguzi.Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.
Imagine huyu anayetoa hiyo hoja alikuwa waziri!! Anaposhauri serikali ijenge hayo maghorofa angekuwa pia anashauri jinsi serikali itakavyopata hizo pesa za kuwalipa hao wazaramo wenzake na za kujengea hayo maghorofa!!Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.
hilo swali hua najiuliza kila siku shida ipo wapi ya kuamua kwamba ujenzi holela sasa marufuku, maana muda unakwenda na ujenzi holela unaendelea tu kwenye miji mpya inayochipukia, na wakati watu wa mipango watu ardhi wapoAna hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etc
factosMada imetawaliwa na chuki za kisiasa. Njia mojawapo ya kuondoa malazi holela ni hio. Kubomoa vinanda vibovu viluvyokaa bila mpangilio na kujenga makazi ya jumuia huku kila aliekuwa na nyumba hapo anapewa nyumba moja.