Jafo: Wakurugenzi watakaoshindwa kupata 50% ya mapato hadi Januari wanaweza kuwekwa pembeni

Jafo: Wakurugenzi watakaoshindwa kupata 50% ya mapato hadi Januari wanaweza kuwekwa pembeni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri 185 nchini kuhakikisha wanafikisha zaidi ya 50% ya makusanyo ya mapato ifikapo Januari 15,2021.

Ametoa agizo hilo wakati akiwasalimia watumishi wa halmashauri ya mji wa Njombe katika ukumbi wa halmashauri hiyo akipita kuelekea mkoani Ruvuma huku akiwataka watakaoshindwa kufika nusu ya lengo wajitafakari.

“Tarehe 15 mwezi wa kwanza nitatoa taarifa ya miezi 6 ya ukusanayaji mapato,wakurugenzi wote wa halmashauri 185 wakajipime wakati wanaenda krismasi sitaki kuona halmashauri yoyote iliyopata chini ya 50%”alisema Waziri Jafo.

Jafo aliongeza kuwa “Halmashauri itakayokuwa imekusanya chini ya 50% mkurugenzi huyo je anafaa kuendelea na serikali ya awamu ya pili ya kipindi cha tano cha Dkt,John Pombe Magufuli ama hatoshi awekwe pembezoni aje mwingine anayeweza kukusanya mapato.”aliongeza Jafo.

Amesema, “Hatutashughulika na wakurugenzi peke yake tutashughulika na watunza hazina pamoja na maafisa mipango,hili ni agizo langu kwa halmashauri zote nchi nzima.'' Aliongeza.

Aidha waziri Jafo ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Njombe na mkurugenzi wake Ally Juma kwa kufanikiwa kuongoza katika taarifa yake iliyoishia jana 21 Disemba ikionyesha Halmashauri hiyo kuongoza kimkoa na kuwa miongozni mwa halmashauri inayofanya vizuri kitaifa.

“Naipongeza halmashauri ya wilaya ya Njombe ambayo mpaka jana tarehe 21 Disember kwenye taarifa yangu wamekusanya bilioni 1.707 sawa na 72% na ni miongoni mwa halmashauri mpaka leo zilizokuwa kinara Tanzania kwa ukusanyaji wa mapato.”alisema Seleman Jafo.

Hata hivyo amesema halmashauri ya Wilaya ya Makete ndiyo inayofanya vibaya mpaka sasa katika mkoa wa Njombe kwa kukusanya milioni 599.

“Taarifa yangu mpaka jana inaonyesha halmashauri ya wilaya ya Makete imekusanya milioni 599 sawa na 25% nje ya bilioni 2.441 kwa hiyo mna kazi kubwa ya madeni.” alisema Jafo.

“Halmsahauri ya mji wa Njombe imekusanya 48% mpaka jana 21 Disemba sawa na 3.299 bilioni tunapomaliza mwezi huu disemba tunatarajia halmashauri zote ziwe zimekusanya sio chini ya 50%.”alisema waziri Jafo.

Mbunge wa jimbo la Njombe mjini Mh,Deodatus Mwanyika amemshukuru waziri Jafo kwa kufika katika halmashauri hiyo na kukagua baadhi ya miradi inayojengwa ndani ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.
 
Qwerty
image_ade680fb-0920-4371-97d6-564012f3af4d20201220_214810.jpeg
image_1416a32d-80ba-4ffc-bb55-07f59767085b20201218_145424.jpeg
 
FB_IMG_1608646257610.jpg


Hayo yamesemwa na Waziri wa Tamisemi Mh Jaffo alipokuwa akiongea mkoani Njombe.

Kwamba kama halmashauri unayoiongoza haijafikia 50% ya makadirio ya makusanyo hadi january basi ni wazi wewe DED utafutwa kazi

Mytake: Kuanzia January wananchi wengi watakiona cha Mtemakuni .
 
Haya matamko ndio yanasababisha mwananchi wa kawaida azidi kuumizwa kwa kodi zisizoeleweka, halafu tena waziri mwingine atakuja aseme amewasimamisha kazi waliobambikia kodi wananchi.

Hawa jamaa wangetuliza vichwa vyao watafute namna bora ya kutawala nchi, huku kukurupuka kwao wanaishia kuichafua serikali tu na kutengeneza chuki kati ya serikali na wananchi.
 
Haya matamko ndio yanasababisha mwananchi wa kawaida azidi kuumizwa kwa kodi zisizoeleweka, halafu tena waziri mwingine atakuja aseme amewasimamisha kazi waliobambikia kodi wananchi
Hii itasaidia sana kwenye kukuza uwekezaji kwenye sekta tofauti kwa wakurugenzi kuhakikisha wanaongeza uwekezaji na wawekezaji wapya pamoja na kuwalinda na kuwasupport wawekezaji waliopo.

Watakua wamepewa target zinazotekelezeka kadri ya halmashauri na sio adhabu.
 
Back
Top Bottom