Ikaria
Member
- Jul 17, 2019
- 93
- 238
Jaji wa Mahakama ya Juu Lawrence Mugambi amepokonywa walinzi wake siku tatu tu baada ya kumhukumu kifungo cha miezi 6 jela Kaimu Inspekta Jenerali Mkuu Gilbert Masengeli, kwa kosa la kudharau mahakama.
Kufuatia kitendo hicho Tume ya Huduma za Mahakama(JSC) ikiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome imehutubia Wanahabari ikitaka Idara ya Polisi kumrejeshea Jaji Lawrence Mugambi walinzi wake mara moja.
Jaji Lawrence alimhukumu IGP Masengeli Ijumaa iliyopita lakini mpaka sasa IGP hajajisalimisha kwa Mkurugenzi wa Idara ya Magereza kama alivyoagizwa na mahakama. Ikumbukwe mahakama iliongeza kuwa iwapo IGP hatojisalimisha, basi Waziri wa Mambo ya ndani Professor Kithure Kindiki atoe agizo la kukamatwa kwake.