Jaji aliyemhukumu IGP Masengeli kifungo jela apokonywa walinzi; Jaji Mkuu Koome ataka warejeshwe mara moja

Jaji aliyemhukumu IGP Masengeli kifungo jela apokonywa walinzi; Jaji Mkuu Koome ataka warejeshwe mara moja

Jaji wa Mahakama ya Juu Lawrence Mugambi amepokonywa walinzi wake siku tatu tu baada ya kumhukumu kifungo cha miezi 6 jela Kaimu Inspekta Jenerali Mkuu Gilbert Masengeli, kwa kosa la kudharau mahakama.

Kufuatia kitendo hicho Tume ya Huduma za Mahakama(JSC) ikiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome imehutubia Wanahabari ikitaka Idara ya Polisi kumrejeshea Jaji Lawrence Mugambi walinzi wake mara moja.

Jaji Lawrence alimhukumu IGP Masengeli Ijumaa iliyopita lakini mpaka sasa IGP hajajisalimisha kwa Mkurugenzi wa Idara ya Magereza kama alivyoagizwa na mahakama. Ikumbukwe mahakama iliongeza kuwa iwapo IGP hatojisalimisha, basi Waziri wa Mambo ya ndani Professor Kithure Kindiki atoe agizo la kukamatwa kwake.

View attachment 3097466View attachment 3097469View attachment 3097471View attachment 3097472
Vipi

Na hii tuilaumu ccm?
 
Huu mchezo wa paka na PANYA 😁😁😁.sema Kenya comedy sana
 
Tanganyika isinge weza hata kujaribu.mahakama ni ccm B.
All the best
 
Kuna watu humu JF huwa wanatwambia Kenya ina Katiba nzuri kuliko Tanzania. Ebu waje watufafanulie uzuri wake hapa.
 
Back
Top Bottom