Jaji Chande Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 asema 'picha baadhi zilikuwa halisi nyingine zilitengenezwa kwa akili unde'

Jaji Chande Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 asema 'picha baadhi zilikuwa halisi nyingine zilitengenezwa kwa akili unde'

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Jaji Chande akiwasilisha ripoti ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, anasema "Jumla ya picha mjongeo 450, picha mjongeo 880, zilikusanywa kwa njia mbalimbali na baadhi zilikuwa zimesambaa mitandaoni kwa zaidi ya mara moja.

Picha hizi zilipatikana na ziliwasilishwa na mashuhuda wa matukio, watoa taarifa wa vyombo vya ulinzi na usalama, na vyanzo vya wazi yaani (Open Source) ikiwemo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Katika kubaini uhalisia wake, baadhi ya picha zilichambuliwa na kufanyiwa uchunguzi wa kisayansi kwa kutumia wataalamu walioidhinishwa. Uchunguzi huo hususan kwa picha zilizokuwa zikizunguka zaidi mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, baadhi yake zilikuwa halisi na za kweli lakini nyingine hazikuwa halisi na zilichezewa kwa kutumia akiliunde na nusu ukweli.

Methodolojia hii iliwezesha tume kutofautisha picha halisi na sio halisi na mfano mmojawapo ni picha ambayo imetumika mara nyingi kuonyesha maiti zikiwa kwenye mifuko ya blue zikizikwa kwenye makaburi ya halaiki. Picha hiyo kwa mujibu wa uchunguzi imekuwa ikitumika sehemu nyingi duniani."



kio​
 

Uchambuzi wa video na picha ulikuwa sehemu kubwa katika uchambuzi wa tume, hususan katika kuelewa madhara ya kibinadamu. Jumla ya picha mnato 450 na picha mjongeo (video) 880 zilikusanywa kwa njia mbalimbali na baadhi zilikuwa zimesambazwa mitandaoni kwa zaidi ya mara moja."

Picha hizi zilipatikana na kuwasilishwa na mashuhuda wa matukio, watoa taarifa, vyombo vya ulinzi na usalama, na vyanzo vya wazi (Open Source) ikiwemo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii."

Katika kubaini uhalisia wake, baadhi ya picha zilichambuliwa na kufanyiwa uchunguzi wa kisayansi kwa kutumia wataalamu walioidhinishwa."

Uchunguzi huo ulibaini kuwa picha nyingi zilizokuwa zikizunguka mitandaoni, baadhi zilikuwa halisi na za kweli, lakini nyingine hazikuwa halisi na zimechezewa kwa kutumia akili mnemba (AI) na nusu ukweli."

Mfano mmojawapo ni picha ambayo imetumiwa mara nyingi kuonyesha miili ikiwa kwenye mifuko ya rangi ya bluu ikizikwa kwenye makaburi ya halaiki. Picha hiyo, kwa mujibu wa uchunguzi, imekuwa ikitumiwa sehemu nyingi duniani. Jaji Chande
 
Back
Top Bottom