Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage ana nafasi nzuri ya kutengeneza historia na hata kupendekezwa kugombea Tuzo ya Amani ya Nobel

Mshana, una maanisha ' Nobel peace prize' ? Kweli? Kwa kipi hasa. Sema unatania ili heshima ulojijegea humu iendelee kutamalaki .
Chaguzi nyingi za Africa huchafuliwa na tume za uchaguzi ..kwasasa hili unaweza kuliona ni jambo dogo sana...lakini katika udogo wake linaweza kupindua historia
 
Shida ni pale unapoona hadi watu wenye akili timamu nao wanasubiri Magufuli kuenguliwa
Mkuu umenifanya nichekee kwa sauti kubwa.

Vijana wa bavicha huwa wanajua kujitoa ufahamu.

Lakini siyo mbaya kujipa matumaini.
 
Andaeni sababu baada ya kushindwa mwezi October. Sio kuota ndoto za alinacha
 
Tuzo ya Amani ya Nobel?
Mzee unaijua hii tuzo vizuri?
Inatolewa kwa mtu aliyesuluhisha Vita au machafuko yaliyokuwepo muda mrefu
Mfano yule Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa kumaliza yale machafuko ya waOromo kipindi kile
Hata huyu kaijage akitenda haki atakuwa emesuluhisha machafuko na vita.
 
Bado mapema, lakini so far utendaji wa Tume umeridhisha ukiondoa uhuni uhuni mdogo mdogo uliofanyanywa na wasimamizi wa chaguzi majimboni na kwenye kata!!
 
Bado mapema, lakini so far utendaji wa Tume umeridhisha ukiondoa uhuni uhuni mdogo mdogo uliofanyanywa na wasimamizi wa chaguzi majimboni na kwenye kata!!
Dalili njema...!?
 
Bandiko Zuri Lenye Hamasa Ya Haki Na Amani....

Hongera kwalo!

Nitofautiane Nawe Kidogo;

Tuzo Ya NOBEL si ya mchezomchezo......

Apewaye Ni Lazima Kuwe Na Jambo Kubwa Alilolifanya "KUENDANA" na MAZINGIRA ya nchi.....

Je Tanzania ni nchi yenye migogoro ya umwagaji damu KISIASA KIDINI NA KIKABILA?!!!

Jibu: HATUJAFIKA HUKO na HATUELEKEI KUFIKA HUKO japo tuna sintofahamu za hapa na pale.....

Simuoni Jaji Wetu Kipenzi Kaijage Kufikiriwa kuwavuta wale NGULI,rafiki zetu na WAHISANI wetu NORWAY kumkabidhi TUZO YA NOBELI......

Wote Waliopata Hiyo Tuzo Hapa Afrika, walikuwa na sababu Nzito na Kuntu mno....

Iwe ni Sirleaf...
Iwe ni Sadat....
Iwe Ni Luthuli....
Iwe Ni Mandela.....


Tanzania Ya Amani,
Tanzania Ya Haki,
Siempre Siempre Tanzania.
 
Mi ninachofurahi Ni kuwa kwa wiki mbili tu lissu ameaza kuondoa uoga uliotamalaki miongoni mwa taasisi za umma na serikali

Mahakama imeanza kujirudi, polisi nao wanalazimika kunyooka, na Sasa tume nao wameanza kunyooka
 
Angalieni presha isije ikawaua. CCM chini ya mhe rais Magufuli, tutashinda kwa kishindo kikubwa sana.

Hivi wanaoweza kufa kwa pressure ni wepi haswa?

Ni hawa ambao wamezoea ushindi haramu na kutoyaelewa maumivu ya kushindwa katika uchaguzi na sasa GIZA LA KUSHINDWA LIKIWA LIMETANDA MBELE YA NYUSO ZAO?

AU

Wale ambao wanayajua machungu ya kushindwa katika uchaguzi na sasa wanaiona NURU YA USHINDI MBELE YAO na hayupo wa kuizima NURU HIYO?

KWA UPANDE MWINGINE;

Hebu fikiri kuhusu tajiri ambaye hajawahi kuonja taabu za umasikini.

NA

Na upande huu mfikirie masikini anayejua machungu na taabu za umaskini. Leo anapata neema ya kuondolewa taabu na mahangaiko yake...

Ni yupi yuko kwenye position ya kufa kwa pressure kutokana na mabadiliko anayopitia ktk maisha yake?

Obviously ni tajiri anayeingia kwenye umasikini!

Sasa weka akili zako kumkichwa ung'amue fumbo hili...
 
[emoji1752][emoji1545][emoji1545][emoji1545]tuzo za Nobel zina madaraja tofauti ...unamkumbuka huyu Mama Wangare Maathai?
 
MSHANA JR, LEO UMEKULA NINI MBONA UNATEMA MADINI SANA. GREAT POST UBARIKIWE.
 
[emoji1752][emoji1545][emoji1545][emoji1545]tuzo za Nobel zina madaraja tofauti ...unamkumbuka huyu Mama Wangare Maathai?
View attachment 1548941

Hakika.....Mama Yetu Kutoka Nchini Kenya.

Mkuu Lakini Kama sikosei Tunamhusisha Jaji Kaijage na TUZO juu ya HAKI AMANI NA MARIDHIANO wakati wa mchakato wa Uchaguzi na Kipindi Cha Matokeo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…