Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage na Tume yako na TCRA acheni kufungia Vyombo vya Habari

Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage na Tume yako na TCRA acheni kufungia Vyombo vya Habari

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Kazi ya Vyombo vya Habari ni kutoa taarifa bila kujalisha taaarifa inahusu nini. Kufungia vyombo vya Habari kwa sababu za kihunihuni ni Uonevu uliovuka Mipaka.

Kama ni Machafuko, anayeweza kuyaleta ni Jaji Kaijage na Tume yako ya uchaguzi. Haiwezekani ninyi mnaengua watu kihuni huni na kuwaondolea haki yao ya kuchaguliwa kwa sababu za kihuni huni alafu msitake vyombo vya habari kuhabarisha huu uhuni wenu.

Yaan nchi nzima CCM ndo wanajua kujaza fomu? Pemba huko wagombea wote wameenguliwa kwa sababu za uhuni uhuni, alafu ninyi badala ya kushugulika na wanaoleta huu uhuni, ninyi mnashugulika na anayetoa taarifa.

Sasa ni hivi, Mimi Msukuma wa Bariadi ndani ndani huku, siwezi kwenda Pemba kufanya machafuko, hayo machafuko yatafanywa na Wapemba wenyewe ambao ndio wanayoshuhudia yanayowatokea huko.

Kufungia vyombo vya habari hakuna athari yoyote kwa wanaotendewa uhuni.

Hii ni kwanini msiache watu washindane? Wananchi wachague Mtu wanayemtaka? Inamaana mnataka kulazimisha mfumo wa chama kimoja?

Kwamba CCM na watu wake ndio wanaojua kujaza fomu? Wanaojua kuweka mapingamizi nakushinda? Kwamba Wakurugenzi ambao ndio chanzo cha haya, hawchukulii hatua bali Vyombo vya Habari? Haya yote ni kwa faida ya nani? Ndio mnataka kumuongezea muhuni wenu muda wa kusalia madarakani?

Kwa dunia ipi? Wajinga nyinyi, Dunia ya leo kuna kiongozi wakubakia salama kwa uhuniuhuni? Nyinyi wapeni watu sababu za kuinuka na kupambania haki zao, alafu ndio mtajua dunia inawatizama, wako wapi walojaribu huu uhuni?

Muhuni wenu huyu, yupo tayari kuona damu ya watanzania inamwaga, kwa sababu ya Uhuni wake wa kudhania kuwa Watanzania milioni 60 wote wanampenda?

Wananchi wanajua kiongozi wao, wanajja nani anawafaa, awe CCM au upinzani kama wananchi hawakuitaji, hawakuitaji tu na wengi wape.

Kwamba Mzee Nyerere alikua mpuuzi sana kukubali mfumo wa vyama vingi na mikataba yake? Mzeee Kikwete, na wewe umekaaa kimyaa, umeungana na CCM na uhuni wake kuikomoa Demokrasia?

Nina Mengi ya kuandika, ila fahamuni haya, mimi Carlos The Jackal , msukuma na daktari kijana Msomi na makini, nisiye na njaa, haitotokea hata siku moja kuielewa CCM na Uhuni wake.

Na hili lazima liheshimiwe katika hiyo Order, hayo madege, mareli, mabarabara, na uovyo ovyo wenu hauwezi nifanya hata siku moja kua kipofu hata nisione Uovu mnaowafanyia wapinzani wenu, Kuua watu, kuteka watu, makesi ya hovyohovyo, ukandamizaji , mateso na manyanyaso.

Nyinyi mtaendelea kupata kura za wanyonge matahira, na waliojitoa ufahamu, wenye njaaa za buku saba, masikini wanaonunuliwa lakini sio mimi na vijana wengine wote walio makini.
 
Unajua, una haki ya kutoa maoni yako na kila mtanzqnia ana haki ya kutoa maoni yake, hata kama ni mabaya kiasi gani, haki hii ni lazima ilindwe, ima faima, pia ni kweli kuwa zipo shetia nyingi na mbaya sana, mradi zipo, sisi wote tunapaswa kuwa makini nazo, na kufanya kila njia; kwanza kutozivunja, pili kuziondoa kwa njia za umma na kwa amani, katika kipindi hiki kigumu kwa Watanzania, ambacho ni sawa tu na vita tuorganiza mambo yetu vizuri na 'tusiantagozize'
 
Tatizo kubwa la chanzo cha uhuni katika uchaguzi hapa nchini ni kukosekana kwa tume huru ambayo inaendesha mambo bila kuingiliwa.
 
Carlos The Jackal,

Taifa ambalo 70%watu wake hawana elimu ya kujitatulia shida zao za kila siku alafu wakutane na uhuru husio na mipaka ni hatari kubwa hivyo kufungia ni jambo bora kabisa hasa nyakati za uchaguzi ambao taarifa za chuki na uzushi ni nyingi kupita maelezo wamestaili ili wengine wajifunze na huyo ni mtoto wa nyumbani sasa nyie wengine endeleeni kupotosha bani itakuwa ni ya mwaka, sisi kama taifa tunaitaji kuweka misingi ya mipaka ya uhuru ndio maana kuna nchi za ulaya wanatamaduni zao na wasifosi tufanane.
 
Carlos The Jackal,

Umeongea ukweli Mungu akubariki ukweli umekuweka huru.

Njaa na umasikini wa akili kwa vijana ndio chanzo cha CCM kutawala na CCM haipo tayari kuondoa umaskini kwasababu ndio mtaji wake.
cc. johnthebaptist. Vijana wa aina yako ndio chanzo cha umasikini Tanzania na dhambi hii ya unafiki itawatafuna mpaka milele, kuweni wazalendo Tanzania ni yetu sote tuseme kweli na tufanye kweli.
 
Taifa ambalo 70%watu wake hawana elimu ya kujitatulia shida zao za kila siku alafu wakutane na uhuru husio na mipaka ni hatari kubwa hivyo kufungia ni jambo bora kabisa hasa nyakati za uchaguzi ambao taarifa za chuki na uzushi ni nyingi kupita maelezo wamestaili ili wengine wajifunze na huyo ni mtoto wa nyumbani sasa nyie wengine endeleeni kupotosha bani itakuwa ni ya mwaka,sisi kama taifa tunaitaji kuweka misingi ya mipaka ya uhuru ndio maana kuna nchi za ulaya wanatamaduni zao na wasifosi tufanane.
Unafungiaje Chombo vha habar kwa kutoa taarifa ya mgombea kupita bila kupingwa et nikuleta machafuko , ili hali kuna mtu kabisa ndio anayechochea haya machafuko? Kwann wasijikite nahawa wanaosababisha vyombo vya habar kutaarifu umma juu ya yale msoyapenda?

Alafu bado unajiona kichwan kwako uko na uzima?

Kwa iyo kufungia chombo, ndio kuepusha machafuko?
 
Taifa ambalo 70%watu wake hawana elimu ya kujitatulia shida zao za kila siku alafu wakutane na uhuru husio na mipaka ni hatari kubwa hivyo kufungia ni jambo bora kabisa hasa nyakati za uchaguzi ambao taarifa za chuki na uzushi ni nyingi kupita maelezo wamestaili ili wengine wajifunze na huyo ni mtoto wa nyumbani sasa nyie wengine endeleeni kupotosha bani itakuwa ni ya mwaka,sisi kama taifa tunaitaji kuweka misingi ya mipaka ya uhuru ndio maana kuna nchi za Ulaya wanatamaduni zao na wasifosi tufanane.
Tatizo ya nchi za zetu za dunia ya tatu watu kama wewe huwa mnadhani mnaishi kwa hisani ya siasa ya watawala hamuishi katika takwa la kikatiba na uzalendo uliotukuka, lazima mseme na kuishi katika misingi ya udharimu ili kuwafurahisha wanaowatuma umaskini umekuwa mpaka katika fikra zenu.

Tanzania ni yetu sote tuache ukweli uonekane ili kutafakari ni wapi tumekosea CCM ipo madarakani miaka 43 imeshindwa kuleta maendeleo ya watu na vitu tuna sera za hovyo zisizokuwa na mwelekeo makini ndio hofu yenu hamtaki uwazi.
 
Kama Daktari ndio una akili za ivo nimejikuta tu nahurumia wagonjwa unao watibu, ntasikitika zaidi nikisikiw kuwa utakuwa umesomeshwa kwa Grants au Scholarship na nchi yako.
 
Umeongea ukweli Mungu akubariki ukweli umekuweka huru.

Njaa na umasikini wa akili kwa vijana ndio chanzo cha CCM kutawala na CCM haipo tayari kuondoa umaskini kwasababu ndio mtaji wake.
cc. johnthebaptist. Vijana wa aina yako ndio chanzo cha umasikini Tanzania na dhambi hii ya unafiki itawatafuna mpaka milele, kuweni wazalendo Tanzania ni yetu sote tuseme kweli na tufanye kweli.
Bwashee mimi siyo kijana

Pili, ukweli unapatikana kwenye Biblia takatifu huku kwenye siasa ni fitna, ulaghai, mizaha na unafiki ndio vinatawala.
 
Back
Top Bottom