Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania


Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

MWANDISHI WA HABARI MSAIDIZI WA RAIS?
hapa nafikiri ni tatizo la lugha yetu labda angeweka mkato kati ya Rais na Msaidizi kwani hata option uliyotoa bado ina mkanganyiko
 
Conflicts of intrest ! Unataka kutwambia kuwa katika familia moja akipata cheo mmoja basi wengine wasfanye kazi serikalini?

Hata mimi hili linanitatiza sana watu wanalalama sana wakiona majina yanafanana. Mnataka kuniambia kama Baba/mama yangu ni Raisi au waziri mkuu mimi sisitahili kufanya kazi popote? au kuwa mtu maarufu?
kama mtu ana uwezo tatizo lipo wapi? tuache majungu lazivyo hii JF itaonekana ni ukumbi ya majungu na mipasho!!!!!

conflict of interest isichanganywe hapa. maana yake ni nini? ingekuwa mtu mmoja ana serve nafasi mbili labda TISS na CJ (au CJ na pia mbunge/waziri) labda tungesema hivyo lakini ni watu wawili tofauti
 
Hongera Chande, kwanza nakupa hongera kama swahib yako, pili nakupa hongera kama mtoto wa mjini Dar. Ntakuja nyumbani kukuletea hongera zangu za dhati, waambie hao maaskari mzee Dar akija wasimletee taabu getini!

punguza mbwembwe.
 
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

MWANDISHI WA HABARI MSAIDIZI WA RAIS?
hapa nafikiri ni tatizo la lugha yetu labda angeweka mkato kati ya Rais na Msaidizi kwani hata option uliyotoa bado ina mkanganyiko

Ni kukosa umakini tu.

Angeweza kuandika:

Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari Msaidizi
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu, Dar es salaam


Mapungufu mengine: haina kichwa cha habari, angeweza kusema: Rais Amteua Othman Chande Jaji Mkuu Mpya Tanzania
 

Thanks for being honesty... "For the second time..." What about other so may "times"???????
 
Mimi nafikiri hakuna tatizo kwani ukiangalia wasifu wa majaji wote watatu waliokuwa wakitajwa utaona kwamba Jaji Chande ana "boasts rich international experience and exposure in the management of judicial affairs" kama the Citizen walivyosema.

Ni "coincidence" tu kwamba kaka mtu ni bosi wa TISS. Tatizo la neno hili ambalo maana yake ni tukio au matukio kutokea kwa wakti mmoja ni kwamba kuna wakti tukio hilo linaweza kuchukua muda kama tunaovyoona kwamba kaka mtu alikwishaukwaa ukurugenzi wa TISS na mdogo pengine akawa nae ana hamu ya kuwa mtu fulani katika Tanzania.

Kuna familia nyingine watoto wanajengwa kwa maneno kama vile kuwa "eminent person" au kuwa "prominent" na yote haya yanamaanisha kwamba wewe utakuwa kwenye nafasi ya juu kwenye jamii na watifuata maneno hayo matokeo yake ni haya ya familia ya akina Othman.

Lakini pia wamesoma kufikia hapo walipo kwahio sioni tatizo kwani nao wanapita hapo na watakuwa wengine ingawa hatufahamu wengine wale wale wa kwenye mzunguko au wapya kabisa.
 
"Ni "coincidence" tu kwamba kaka mtu ni bosi wa TISS. Tatizo la neno hili ambalo maana yake ni tukio au matukio kutokea kwa wakti mmoja ni kwamba kuna wakti tukio hilo linaweza kuchukua muda kama tunaovyoona kwamba kaka mtu alikwishaukwaa ukurugenzi wa TISS na mdogo pengine akawa nae ana hamu ya kuwa mtu fulani katika Tanzania."

Bw. Richard na wengineo who went to school and can actually read and understand!!!!...
For the umpteenth time, hawa jamaa SIO NDUGU KABISA..... The newspaper report got it totally wrong here!
Ni wazawa wa Tanga. Rashid Othman is actually much younger than judge Moh'd Chande.
 
..kuna mtu anafahamu hukumu yoyote ile significant ambayo imewahi kutolewa na Chief Justice Chande?

..huwezi kumpinga wala kumkubali bila kutumia HUKUMU or LEGAL OPINIONS alizopata kutoa.
 
Katiba mpya, hapa ndio tunaona why Tanzania need new Katiba. Kuna siku kuna raisi atatuchagualia jaji mkuu kisa ni kimada wake kama hii katiba itaendelea kumpa rungu raisi.

Mwisho wa huu upuzi. Tunaka vetting process, kama raisi anapendekeza jina then jina linapelekwa bungeni, kabla ya kupigiwa kura anatakiwa kufanya majohojiano (open door) na kamati ya bunge inayohusika na mambo ya sheria. Kisha kura zinapigwa na bunge kwa 50% over.

Lazima tuzibe mianya ya kuchaguliwa jiji kaptula au sketi.
 

Wakati mwingine huwa napata wasiwasi kuwa Waandishi wa Magazeti yetu baadhi yao wanakuwa wachochezi na watu wa fitna,kuna umuhimu wa kuhakiki habari zao.Jaji Mkuu mteule hana mahusiano yoyote ya kindugu na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa
 
ili kusave muda naomba utuambie mtoa mada amedanganya wapi je hawa jamaa sio ndugu??????

hawa jamaa hawana undugu kabisaaaaaa, hilo jina la othman ndilo lilowachanganya. Watu wanaifanya jf kama sio ya great thinkers kwa kuandika vitu ambavyo havina upembuzi yakinifu, tuumize vichwa jamani......as great thinkers.
 

Mkuu usisahau pia kwamba J.F Kennedy alimteua mdogo wake Bobby Kennedy kuwa Attorney General.. na kazi zilienda fresh tu!
 
Mkuu usisahau pia kwamba J.F Kennedy alimteua mdogo wake Bobby Kennedy kuwa Attorney General.. na kazi zilienda fresh tu!
Lakini baada ya hapo Wamarekani wakabadilisha sheria. Hakuna cha kuteua ndugu, mjomba, etc katika kazi za serikali.
 
Itafika kipindi wapogoro na wamakonde nao watadai hawapewi nafasi katika timu ya taifa ya riadha! ati imejaa watu wa kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Singida! Mtu ateuliwe kutokana na kuwa na vigezo vya uwezo vya kuwazidi wenzake wooooooote siyo eti kwa sababu kabla yake hakujawahi kutokea mtu wa kabila lake au dini yake au jinsia yake, la sivyo nchi hii tunaiangamiza!na hatutaendelea tutazidi kuwa maskini milele!
 


Duh!

hivi wewe ni mtaalam katika fani hii au ndio kutaka sifa tuu?
 
hawa jamaa hawana undugu kabisaaaaaa, hilo jina la othman ndilo lilowachanganya. Watu wanaifanya jf kama sio ya great thinkers kwa kuandika vitu ambavyo havina upembuzi yakinifu, tuumize vichwa jamani......as great thinkers.

Hata mimi nimepata habari za kuaminika kutoka kwa mtu anayemfahamu Othman wa TISS mpaka kwao amesema kuwa siyo ndugu. Kama wangekuwa ndugu lazima angemfaham Mh. Chande kwa vile anaifahamu familia ya kina Othman vizuri sana.

Ila bila ushabiki wa kidini, CV ya jamaa imetulia kuliko za hawa jamaa zetu ambao wamekulia kwenye hii system ya rushwa.
 

Hili Bunge letu ni joka la Kibisa. Ulishaona wapi joka la Kibisa linauma wacheza ngoma au hata watazamaji?
 

Kwa elimu na uzoefu wa Mheshimiwa Othman mimi naona anastahili kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Ila hawa watu wanaoongelea uislam na ukristo hivi mbona huwa hawakumbuki waumini wa dini za asili au wale wasioamini katika hizi dini za kiarabu na kizungu?. Je ina maana wenyewe hawana haki nchi hii? Tukumbuke kuwa hii nchi ni yetu wote bila kujali dini, rangi, kabila wala wlimu ya mtu.
 
Endeleni tu na porojo huyo yopo kwa ajili ya CCM na sio vigenevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…