Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania

Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania

Msiangushe udini huyu jaji anafaa, ila tatizo langu lipo kwa huyo aliyeandika taarifa hii. Mbona amejitaja kama MWANDISHI WA HABARI WA RAIS MSAIDIZI. Hapa kuna uhakika kweli? Tuna Rais Msaidizi? Au angetakiwa kusema ni MWANDISHI WA HABARI MSAIDIZI WA RAIS? Kweli tutaona mengi mwaka huu na ujao.

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

MWANDISHI WA HABARI MSAIDIZI WA RAIS?
hapa nafikiri ni tatizo la lugha yetu labda angeweka mkato kati ya Rais na Msaidizi kwani hata option uliyotoa bado ina mkanganyiko
 
Conflicts of intrest ! Unataka kutwambia kuwa katika familia moja akipata cheo mmoja basi wengine wasfanye kazi serikalini?

Hata mimi hili linanitatiza sana watu wanalalama sana wakiona majina yanafanana. Mnataka kuniambia kama Baba/mama yangu ni Raisi au waziri mkuu mimi sisitahili kufanya kazi popote? au kuwa mtu maarufu?
kama mtu ana uwezo tatizo lipo wapi? tuache majungu lazivyo hii JF itaonekana ni ukumbi ya majungu na mipasho!!!!!

conflict of interest isichanganywe hapa. maana yake ni nini? ingekuwa mtu mmoja ana serve nafasi mbili labda TISS na CJ (au CJ na pia mbunge/waziri) labda tungesema hivyo lakini ni watu wawili tofauti
 
Hongera Chande, kwanza nakupa hongera kama swahib yako, pili nakupa hongera kama mtoto wa mjini Dar. Ntakuja nyumbani kukuletea hongera zangu za dhati, waambie hao maaskari mzee Dar akija wasimletee taabu getini!

punguza mbwembwe.
 
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

MWANDISHI WA HABARI MSAIDIZI WA RAIS?
hapa nafikiri ni tatizo la lugha yetu labda angeweka mkato kati ya Rais na Msaidizi kwani hata option uliyotoa bado ina mkanganyiko

Ni kukosa umakini tu.

Angeweza kuandika:

Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari Msaidizi
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu, Dar es salaam


Mapungufu mengine: haina kichwa cha habari, angeweza kusema: Rais Amteua Othman Chande Jaji Mkuu Mpya Tanzania
 
Othman ni mwanasheria mzuri competent among all three names, well he has international and local experience.

JK for the second time you made a good choice kama ulivyofanya first time kwa Magufuli

Mengine yote ni Udini tu taratibu watazoea tu..ukumbuke tangu uhuru 1961 ni wale wale tu..

Watazoea na kwamba Tanzania ni wote sote (kila moja)

Thanks for being honesty... "For the second time..." What about other so may "times"???????
 
Mimi nafikiri hakuna tatizo kwani ukiangalia wasifu wa majaji wote watatu waliokuwa wakitajwa utaona kwamba Jaji Chande ana "boasts rich international experience and exposure in the management of judicial affairs" kama the Citizen walivyosema.

Ni "coincidence" tu kwamba kaka mtu ni bosi wa TISS. Tatizo la neno hili ambalo maana yake ni tukio au matukio kutokea kwa wakti mmoja ni kwamba kuna wakti tukio hilo linaweza kuchukua muda kama tunaovyoona kwamba kaka mtu alikwishaukwaa ukurugenzi wa TISS na mdogo pengine akawa nae ana hamu ya kuwa mtu fulani katika Tanzania.

Kuna familia nyingine watoto wanajengwa kwa maneno kama vile kuwa "eminent person" au kuwa "prominent" na yote haya yanamaanisha kwamba wewe utakuwa kwenye nafasi ya juu kwenye jamii na watifuata maneno hayo matokeo yake ni haya ya familia ya akina Othman.

Lakini pia wamesoma kufikia hapo walipo kwahio sioni tatizo kwani nao wanapita hapo na watakuwa wengine ingawa hatufahamu wengine wale wale wa kwenye mzunguko au wapya kabisa.
 
"Ni "coincidence" tu kwamba kaka mtu ni bosi wa TISS. Tatizo la neno hili ambalo maana yake ni tukio au matukio kutokea kwa wakti mmoja ni kwamba kuna wakti tukio hilo linaweza kuchukua muda kama tunaovyoona kwamba kaka mtu alikwishaukwaa ukurugenzi wa TISS na mdogo pengine akawa nae ana hamu ya kuwa mtu fulani katika Tanzania."

Bw. Richard na wengineo who went to school and can actually read and understand!!!!...
For the umpteenth time, hawa jamaa SIO NDUGU KABISA..... The newspaper report got it totally wrong here!
Ni wazawa wa Tanga. Rashid Othman is actually much younger than judge Moh'd Chande.
 
..kuna mtu anafahamu hukumu yoyote ile significant ambayo imewahi kutolewa na Chief Justice Chande?

..huwezi kumpinga wala kumkubali bila kutumia HUKUMU or LEGAL OPINIONS alizopata kutoa.
 
Katiba mpya, hapa ndio tunaona why Tanzania need new Katiba. Kuna siku kuna raisi atatuchagualia jaji mkuu kisa ni kimada wake kama hii katiba itaendelea kumpa rungu raisi.

Mwisho wa huu upuzi. Tunaka vetting process, kama raisi anapendekeza jina then jina linapelekwa bungeni, kabla ya kupigiwa kura anatakiwa kufanya majohojiano (open door) na kamati ya bunge inayohusika na mambo ya sheria. Kisha kura zinapigwa na bunge kwa 50% over.

Lazima tuzibe mianya ya kuchaguliwa jiji kaptula au sketi.
 
"Ni "coincidence" tu kwamba kaka mtu ni bosi wa TISS. Tatizo la neno hili ambalo maana yake ni tukio au matukio kutokea kwa wakti mmoja ni kwamba kuna wakti tukio hilo linaweza kuchukua muda kama tunaovyoona kwamba kaka mtu alikwishaukwaa ukurugenzi wa TISS na mdogo pengine akawa nae ana hamu ya kuwa mtu fulani katika Tanzania."

Bw. Richard na wengineo who went to school and can actually read and understand!!!!...
For the umpteenth time, hawa jamaa SIO NDUGU KABISA..... The newspaper report got it totally wrong here!
Ni wazawa wa Tanga. Rashid Othman is actually much younger than judge Moh'd Chande.

Wakati mwingine huwa napata wasiwasi kuwa Waandishi wa Magazeti yetu baadhi yao wanakuwa wachochezi na watu wa fitna,kuna umuhimu wa kuhakiki habari zao.Jaji Mkuu mteule hana mahusiano yoyote ya kindugu na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa
 
ili kusave muda naomba utuambie mtoa mada amedanganya wapi je hawa jamaa sio ndugu??????

hawa jamaa hawana undugu kabisaaaaaa, hilo jina la othman ndilo lilowachanganya. Watu wanaifanya jf kama sio ya great thinkers kwa kuandika vitu ambavyo havina upembuzi yakinifu, tuumize vichwa jamani......as great thinkers.
 
Ifike mahala tuache kutia nyongo kila jambo linalofanywa na watawala. Nimesoma kwa makini wasifu wa Jaji Mkuu mpya Othman Chande. Inajitokeza waziwazi kwamba huyu ni mtu mwenye wasifu na sifa za juu kabisa katika maswala ya sheria na mahakama. Ana uzoefu wa hali ya juu kitaifa na kimataifa. Mamlaka ya uteuzi wangekuwa ni wajinga kama wangemuacha kwa sababu tu kaka yake ni Mkurugenzi Mkuu wa TISS. Tony Blair na Gordon Brown waliwahi kuwateua mtu na mdogo wake kuwa katika baraza la mawaziri. Juzijuzi Chama cha Labour kiliwapitisha mtu na kakake kugombea nafasi ya Kiongozi wa labour.

Ni ujuha na ujinga kumteua mtu kwa sababu ya dini, udugu, ukabila, n.k. Vilevile ni ujuha na ujinga wa kutisha kuacha kumteua mtu kwa sababu tu ndugu yake alishatangulia huko serikalini hata kama ana sifa. Haya mambo ya ku-balance kidini, kikabila, kidugu, kikanda na kimokoa ndiyo yanaletekeza mijitu mingine kuteuliwa kuwa mawaziri hata kama haina sifa ili wateuzi waonekane walizingatia mgawanyo wa kimkoa, kidini, kikabila, n.k. Kama mtu ana sifa basi ateuliwa, na kama hakuna mtu mwenye sifa kwa nafasi husika kutoka hiyo dini au kabila au mkoa basi na iwe hivyo. Si lazima kila dini au mkoa uwakilishwe katika nafasi za uteuzi.

Othman Chande, chapa kazi. Una nafasi ya kujitengenezea legacy ya pekee kwa kutoa msukumo muhimu ili hatimaye nchi yetu iwe na Katiba Mpya yenye kuzingatia misingi ya demokrasia na haki za binadamu.

Mkuu usisahau pia kwamba J.F Kennedy alimteua mdogo wake Bobby Kennedy kuwa Attorney General.. na kazi zilienda fresh tu!
 
Mkuu usisahau pia kwamba J.F Kennedy alimteua mdogo wake Bobby Kennedy kuwa Attorney General.. na kazi zilienda fresh tu!
Lakini baada ya hapo Wamarekani wakabadilisha sheria. Hakuna cha kuteua ndugu, mjomba, etc katika kazi za serikali.
 
Itafika kipindi wapogoro na wamakonde nao watadai hawapewi nafasi katika timu ya taifa ya riadha! ati imejaa watu wa kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Singida! Mtu ateuliwe kutokana na kuwa na vigezo vya uwezo vya kuwazidi wenzake wooooooote siyo eti kwa sababu kabla yake hakujawahi kutokea mtu wa kabila lake au dini yake au jinsia yake, la sivyo nchi hii tunaiangamiza!na hatutaendelea tutazidi kuwa maskini milele!
 
Lakini kumchagua Jaji Othman kuwa Jaji Mkuu haitoshi considering judiciary yetu ilivyogawanyika. Infact kwa nini watu hawajiulizi about the exclusivity ya Ukabila uliopo ndani ya Judiciary?

Of course kama tutakuwa hatuko makini kwenye kujadili hili itakuwa yale yalee ya sweeping statements kama vile 'ohhh WACHAGGA wamejazana kwenye judiciary ndio maana kuna nuka rushwa' lakini hakuna anayetaka kuangalia chanzo cha hili. Its quite unfortunate kuwa hata hao the so called University Students hawaji kuchangamsha hili baraza rightly or wrongly kutuelezea tena kwa sababu za kisomi kwa nini Judiciary yetu iko ONE SIDED.......maana kushakuwa so polarised humu and I can also understand pessimism kama ipo.

Nadhani kuna myriad factors ambazo tunaweza kusema kuwa zimeweza ku produce a Tanzanian judiciary with kwa mtazamo wa karibu ni haki kusema kuwa ni:

1.distinctly elite

2.non-representative demographics.

3.Born into families of wealth and privilege

4. Ivy League types

Hiyo point ya 4 ni muhimu kuifafanua kwa sababu most of our judges received their basic education good schools, their law training from either UK or U.S (Mara nyingi ni from the Golden Triangle ya UK ambayo inacombine:OXFORD na CAMBRIDGE, kwa upande mmoja, upande wa pili ni Vyuo ambavyo viko chini ya University of London kama KINGS COLLEGE, LONDON SCHOOL OF ECONOMICS, IMPERIAL COLLEGE na ukiangalia kwa sana utaona the others wamesomea kwenye Ivy League za North East wenyewe wanaziita ambazo kuna BROWN COLUMBIA, CORNELL,DARTMOUTH,HARVARD,PRINCETON na bila kusahau UPENN...hivyo piga ua utaona majaji wakuu wetu hawakoso at least a degree from the above institutions.

Sasa after that wengine waliobtain coveted pupilage at a prominent chambers of barristers kwa waliosoma UK. Na after a long and financially rewarding careers at the highest ranks of the bar, including appointments mbali mbali ndipo hawa waheshimiwa waliiingia kwenye full-time judiciary at the end of their practicing career.Given formal eligibility requirements, informal entrance barriers, and other restrictions, the Tanzania bench is overwhelmingly comprised of mainly older males (kwa sababu ya mfumo dume), Christian and from the most privileged stratum of society. So mtu kama Jaji Othman kuwa Jaji mkuu will always bring eyebrows kwa sababu HE DOESNT FIT THE PROFILE. Thats why nimesema kuwa tokana inbalance tulionayo katika Jamii Rais amefanya uamuzi wa busara kwani anaondoa zile stereotypes kuwa Mswahili tena Muislam hawezi kuwa Jaji mkuu na akatoa Haki sawa kwa wote. Mchukieni tuu Jakana lakini on this, I give him big up japo kama nilivyoelezea kuwa hii fani iko very elitist huko juu .


Yes najua kutakuwa na defenders wa mfumo huu au Judiciary yetu as it is lakini ukweli itabaki pale pale kuwa our Judiciary is SOCIALLY BIASED pili iko OUT OF TOUCH WITH ORDINARY LIVES na mbaya zaidi it LACKS PUBLIC CONFIDENCE THAT JUSTICE IS FAIRLY DISPENSED. Sasa kama mnataka tu we na mjadala ambao utaangalia beyong personalities sawa lakini upande wangu nadhani kuna umuhimu wa kufanya reform katika mhimili huu muhimu kwetu kama taifa kwaili kuongeza vitu vitatu:

1. TRANSPARENCY

2. ACCOUNTABILITY

3. DIVERSITY

Naweza kusema kuwa Post Cold War na mpaka miaka ya hivi karibuni kumekuwa na various 'forces' ambao wamekuwa wakitaka kuwepo kwa reforms ambazo zingeangalia au zingeshed light on issues kama vile a) appointment process b)adopting modern personnel management techniques andof course diversifying the bench to more fairly reflect the general population ili kuondoa minongono (rightly or wrongly) kuwa Wachagga au Wakristo wamejikita kwenye hili eneo/ Ninavyofahamu mimi kuwa pressure inatoka from within kwa maana Tanganyika Law Society, and non- legal professionals and governmental actors (kisirisiri au in private) as well as a broad range of social critics such as SHIVJIS and the like na pia bila kusahau SERIOUS press na bila kusahau wale vocal academics.

Its common ukimuuliza mtu wa mtaani atakuwambia kuwa issues zinazochefua judiciary yetu ni 1.criticisms of insider-preferences

2.political cronyism,

3. na bila kusahau the antiquated appointment system


Anyway najua Jaji Othman atakuwa na kazi kubwa ila kama nikipata nafasi ya kuzungumza naye nitamshauri azingatie mambo matatu na si mengine bali nilishatya mention na ndio yata underline reforms zozote tutakazo kuwa nazo kwenye judiciary nazo ni

1. TRANSPARENCY

2. ACCOUNTABILITY

3. DIVERSITY

Mniwie radhi post yangu ndefu kiasi lakini nimeona si vijabaya nikaongezea hayo niliyoyasema hapo awali


Duh!

hivi wewe ni mtaalam katika fani hii au ndio kutaka sifa tuu?
 
hawa jamaa hawana undugu kabisaaaaaa, hilo jina la othman ndilo lilowachanganya. Watu wanaifanya jf kama sio ya great thinkers kwa kuandika vitu ambavyo havina upembuzi yakinifu, tuumize vichwa jamani......as great thinkers.

Hata mimi nimepata habari za kuaminika kutoka kwa mtu anayemfahamu Othman wa TISS mpaka kwao amesema kuwa siyo ndugu. Kama wangekuwa ndugu lazima angemfaham Mh. Chande kwa vile anaifahamu familia ya kina Othman vizuri sana.

Ila bila ushabiki wa kidini, CV ya jamaa imetulia kuliko za hawa jamaa zetu ambao wamekulia kwenye hii system ya rushwa.
 
Ni mtu mwenye akili zenye kuenea kwenye kizibo cha soda tu ndie anaweza asione walakini kwenye huu uteuzi!
Kwa suala la udini kwangu sidhani kama lipo ILA ni wehu wa hali ya juu kuwapa ndugu wawili (kama kweli ni ndugu kama inavyosemwa) nyadhifa sensitive kama hizi. i.e. Directore wa Usalama wa taifa na jaji mkuu. Inabidi bunge liingilie kati mapema sana kabla mambo hayajaharibika!!

Hili Bunge letu ni joka la Kibisa. Ulishaona wapi joka la Kibisa linauma wacheza ngoma au hata watazamaji?
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425




PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 DIsemba, 2010.

Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.
Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.

Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.

Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Ikulu
Dar es Salaam
26 Disemba, 2010


Kwa elimu na uzoefu wa Mheshimiwa Othman mimi naona anastahili kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Ila hawa watu wanaoongelea uislam na ukristo hivi mbona huwa hawakumbuki waumini wa dini za asili au wale wasioamini katika hizi dini za kiarabu na kizungu?. Je ina maana wenyewe hawana haki nchi hii? Tukumbuke kuwa hii nchi ni yetu wote bila kujali dini, rangi, kabila wala wlimu ya mtu.
 
Endeleni tu na porojo huyo yopo kwa ajili ya CCM na sio vigenevyo.
 
Back
Top Bottom