Hiyo conflict of interest unaona wewe lakini tukisema kwamba UTEUZI WOWOTE WA CCM NI SHARTI KUFWATE MKONDO FULANI na kwamba BILA VIJI-CONNECTIONS FULANI tunduni haujapita wengini wakawa wanadhani ni utani hapa.
Ni wachache mno wanaotazamwa kwa elimu, ufanisi wa kazi na uzalendo wake. Tukisema Dr Malecela kuna Katapila nyuma kama godfather hamsikii. Sasa ya Othman Chande wa TISS kutumia nafasi yake ya sasa kumpigia chapuo mtoto walioachiana ziwa wewe unaona shida gan??? Hata Jaji Makame majuzi alipofanya vizuri kwenye uchaguzi wetu mkuu tayari dogo lake Prof Makame yuko ndani ya ulingo Dodoma anakula good-time kwa 'Hundi ya Wazi' aliouandika kaka kule Tume ya Uchaguzi 2010.
Kwa kifupi, hapa ni Mega-Corruption Syndication, Nepotism, Favouritism and Bird-Feathering kwa kwenda mbele. Kaka JK kanyaga twende!!! Hapa hata gunia la mkaa linaweza kuteuliwa. Wala sitoshangaa Mzee Jangara akiteuliwa Balozi wetu kule Umoja wa Mataifa; kama ni kiingereza atajisomeaga huko huko kazini.
Hivi ndivyo mambo yanavyokwenda baba. Lile swali la rais wa zamani wa Marekani juu ya mtu kujiuliza ataifanyia nini taifa lake; hapa kwetu swali hilo ni kwamba MTU UMEWAHI KUKIFANYIA CCM AU NDUGU YAKO YUPI AMBAYE AMEWAHI KUIFANYIA NINI CCM na wala kuifanyia nini taifa na maslahi yake.
Bwanae, kwenye KATIBA MPYA HUKO rais apunguziwe kwa sana madaraka ya kupindukia kiasi hiki. There is too much President in our everyday lives. Nafasi hizi zote zitangazwe, mashirika makubwa na ya kuaminiko kwenye mambo ya ajira yashirikishwe kama mashirika matatu hivi kila kimoja kikifanya kazi yake kwa peke yake lakini kwa kipidi kimoja.
Mashirika haya yachuje majina kiutaalam bila kuingiliwa, kisha kila muombaji nafasi apewe mi-alama au marks kabla ya kupelekwa majina yaliochujwa (kama 6 hivi kwa nafasi husika) kupelekwa bungeni nako wakabakishwa watatu na kupewa alama mle upya na mwisho rais kupata mtu pale kwa nafasi husika.
Process itakapokua very transparent and most rigorous then accountability to the general publi and not merely the president will be most assured than is the case to-date.
Hivi hawa ni wale watoto wa yule Chande wa kwenye historia kuwemo kwenye Baraza la Mawaziri sio??? Ukweli ni kwamba maendeleo ya nchi hutegemea sana ufanisi wa taasisi zake.
Nako pia ufanisi huo ni lazima utokane na kiwango cha ubora katika kupatikana watendaji hawa. Sasa, tofauti na hapo ni makida makida tu twende kasi!!!
Nimeyakubali mawazo yako mkuu!