EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Sidhani kuna kitu cha kubishania hapa! ..wenzetu wanapojadili teuzi za majaji huchunguza HUKUMU walizotoa, OPINIONS zilizoko ktk maandishi ya mhusika. Hiyo dini sijui inaingiaje hapa, labda kama aliyemteua ndo awe na ajenda yake siri ambayo hata hivyo hatuwezi kuithibitisha hapa. Cha muhimu hapa ni huyu jamaa kuwa independent kwenye maamuzi ya kama CJ bila kuogopa pressure za the big men in power kama alivyofanya mtangulizi wake kwenye kesi ya katiba!
Nakubaliana na wewe mkuu. Ishu ya kawaida watu wanaifanya ya kidini au ya kisiasa. Mbona huko nyuma waislamu hawajawahi kulalamika kutokuwa na na jaji mkuu muislamu? Mimi mkristo lakini hii style ya kujadili mambo kidini inanikera sana. Na hawa watu wanaopiga kelele juu ya huyu jaji hawajawahi kusoma hata hukumu moja ya huyo jaji. Huyu jaji kwanza alikuwa kule east timor akiwatetea wakatoliki dhidi ya waislamu wa Indonesia. Kabla ya kupiga kelele katafute kesi zote alizozitolea huku huyu jaji tokea akiwa hakimu, jaji wa mahakama kuu na na jaji wa mahakama ya rufaa halafu compare na kesi za hao waliotemwa then come back. Vipi angechaguliwa Profesa Issa Shivji kuwa jaji mkuu bado mmgepiga kelele kuwa sio mkristu? Hivi karibuni forum imezidisha udini mpaka inaboa.