JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Kigoma, Lameck Mlacha amewataka Mahakimu kutumia sheria ya kifungo cha nje kwa makosa chini ya miaka mitatu kama ilivyoanishwa katika sheria ili kupunguza mrundikano wa wafungwa gerezani.
Ametoa mfano baadhi ya makosa hayo ni yale madogo na ambayo sio sugu, pia imeelezwa kuwa jamii haina uelewa kuhusu aina hiyo ya adhabu, wengi wakiamini mfungwa lazima atumikie kifungo chake gerezani.
“Adhabu mbadala haitolewi kiholela kwa kuwa inaweza kuathiri jamii, miaka mitatu si kigezo pekee, inatakiwa kuangaliwa jamii ina taswira gani kuhusu kosa husika na rekodi ya mtuhumiwa,” - Jaji Mlacha.