Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madalali Juni 30, 2026 amesema hatarajii kuona viongozi wa kisiasa wakiingilia utendaji wa shughuli za kisheria kwa kigezo cha nyadhifa walizonazo katika kamati za ulinzi na usalama za mikoa au wilaya.
"Mimi nisingependa viongozi wa kisiasa waingilie utendaji wa shughuli zenu [Majaji] kwa vigezo kwamba wao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa au wilaya. Sheria inayowasilisha madaraka yao haikuwapa mamlaka hayo... Hatuwezi kuwa, kama mahakama imeshatoa amri halafu mtu mwingine anakwenda kuzuia. Hiyo ni mahakama au ni kitu gani? Lazima tutofautishe shughuli za kisiasa na shughuli za kisheria na maamuzi yanayofanywa na mahakama."
"Kama sisi tutataka tusiingiliwe, na sisi tuwe wasafi. Sisi wenyewe tuwe wasafi. Tutekeleze wajibu wetu kwa mujibu wa katiba, sheria, maadili na kanuni tulizojiwekea ili tusitoe fursa kwa hao..."