Jaji Mkuu ameiabisha Mahakama na kuwakosea watanzania

Jaji Mkuu ameiabisha Mahakama na kuwakosea watanzania

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
1,679
Reaction score
2,016
Juzi zilitoka habari kwenye mitandao kuwa jaji mkuu wa Tanzania anawalaumu wapelelezi wa kesi mbalimbali kuwa ndio wakutupiwa lawama kwa mlundikano wa wafungwa na kuahirishwa kwa kesi mbalimbali na mahakama.

Tena alienda mbali na kuwalaumu kuwa huwa wanaotoa sababu za Hovyo na zisizo na mashiko.

Nisiseme uwongo nimeshangaa Sana jaji mkuu kuongea kitu Kama hicho ni bora kabisa angekaa kimya kuficha auburn yake.

Hebu tufikili kidogo. Mtu ana kesi tena kesi yenyewe mbaya na wengine wamenyimwa dhamana maana yake wanasota ndani kwa maumivu makali.

Anakuja wakili wa serikali nasababu ya hovyo na isio na mashiko akiomba kesi ihairishwe, wewe Kama jaji ambae umeaminiwa kutoa haki unagundua kabisa kuwa sababu hii ni ya ovyo tena haina mashiko lkn wewe jaji unaamua kwa makusudi kabisa kuahirisha kesi hiyo, bila sababbu ya msingi hivi hapo ni Nani wants kulaumiwa?

Yaani wakili wa Serikali amekupa sababu ya hovyo isiyokua na mashiko lkn wewe ukiwa Msomi kabisa unagundua kuwa hii ni sababbu dhaifu, tena ya hovyo isio kuwa na mashiko lkn unakubaliana nae, hivi Kati yenu ninyi wawili yaani wakili wa serikali na wewe jaji Nani ni wachache hovyo?

Kwa mtizamo wangu wewe jaji uliyegundia kuwa sababu hii ni ya hovyo isiyo na mashiko na wakati huohuo umepewa mamlaka ya kuifuta kesi hiyo lkn bado ukakubaliana na huyu mtu aliyekuletea sababbu dhaifu, za hovyo na zisizokua na mashiko basi wewe ndiye wa hovyo zaidi kuliko huyo aliye kuletea hizo sababbu

Tukumbuke mfano alio utoa Mwl Nyerere kati ya mtu mwenye almasi na mwizi mwenye vichupa na utapata majibu.
 
Tanzania hakuna Mahakama na Bunge bali kuna mhimili uliojichimbia kufanya maamuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kauli ningekuwa wewe nimgeifuta na kuapologise! Ni kauli ya ovyo kabisa. Tujifunze kuwa ratioal na kuargue kama great thinkers. Sidhani kama umewaza hata kidogo kabla ya kutoa kauli hii. Usipende kuangalia kila kitu katika mlengo wa kisiasa. Take your time nenda Mahakani hata wiki moja au fuatilia Bunge ukiwa out of political context uone kama ulikuwa sahihi kuandika hicho ulichoandika!
 
Hii nchi inahitaji mapambano mazito tofauti na hapo tutakuwa watumwa wa watawala au hata wake zao kabisa maana haiwezekani mtu akuteke ,akae na wewe siku tatu chumbani kwake,aibuke akiri kuwa ni yeye anakushikilia,baadae akanushe na kesho saa tano asubuhi anakupeleka mahakamani kwa kesi ya kutengeneza isiyo na dhamana
 
January 6, 2020

Wakili Msomi atoa somo juu ya Mamlaka na Wajibu wa Mahakama Kuu kuhakikisha haki inapatikana na kudhibiti mihimili mingine isivunje Katiba.

Fatma Karume wakili mbobezi aliyesajiliwa na Mahakama Kuu aelezea umuhimu wa Mahakama kujijengea heshima, kuanzia uteuzi wa majaji, jinsi bajeti ya kuendesha mahakama inavyotengwa, Mahakama kutenda haki si tu kama inavyotamkwa na Katiba bali mbele ya umma ionekane inatenda haki....
 
Mahakama kusajili kesi ambazo haijulikani upelelezi wake utaisha lini huku mtuhumiwa akiwa gerezani ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Huwezi amua tu kumshitaki mtu ukijua huna ushahidi unaotosheleza kuithibitishia mahakama.

Dhamana ziwe wazi kwa kesi zote uone kama kutakuwa na kesi za kipumbavu huko mahakamani.

Na hivi watu hawawezi fungua kesi za fidia hasa dhidi ya serikali basi ndio imekuwa shida tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni miongoni mwa watu kadhaa watakaokuja kufungwa huko mbele
 
Yaani hii ni sawa na dereva wa daladala kugombana na konda ati kwanini anashusha watu mahali pasipo kituo, halikuwa usukani na breki anao mwenyewe😂😂
 
Hii kauli ningekuwa wewe nimgeifuta na kuapologise! Ni kauli ya ovyo kabisa. Tujifunze kuwa ratioal na kuargue kama great thinkers. Sidhani kama umewaza hata kidogo kabla ya kutoa kauli hii. Usipende kuangalia kila kitu katika mlengo wa kisiasa. Take your time nenda Mahakani hata wiki moja au fuatilia Bunge ukiwa out of political context uone kama ulikuwa sahihi kuandika hicho ulichoandika!

Mimi ningekuwa wewe hii post yako angalau ninge-edit kama sio kuifuta kabisa. Bunge ni by definition ni political entity, kwa hivyo haiwezekani mtu mwenye akili timamu kulifuatilia out of political context (atalifuatilia kwa context gani sasa, ya kidini?).
 
Back
Top Bottom