Kwanza nampongeza Jaji Masaju kwa kuaminiwa na Mhe. Rais na kumteua kuwa Jaji Mkuu mpya wa Tanzania.
Mara baada ya kula kiapo tunashauri aanze na mambo yafuatayo;_
1. Ondoa uonevu na upendeleo ndani ya muhimili wenyewe, jenga umoja na mshikamano. tenda haki kwa watumishi wote bila upendeleo wala ubaguzi (ndani ya mhimili).
2. Usikubali kuyumbishwa na wakongwe/wafitini na wapiga majungu. Jitenga na fitina na majungu.
3. Rudisha imani na matumaini kwa walio poteza matumaini. haswa watumishi wa chini ndani ya mhimili.
4. Kuwa mkali kwa mambo ya msingi, ili kujenga nidhamu na heshima ya muhimili. Kamwe usiwe mpole watakukupotosha.
5. Hakikisha mahakama zote kuanzia mahakama ya mwanzo hadi mahaka ya Rufaa zinatumia lugha ya Taifa ya Kiswahili katika kusikiliza kesi na kutoa hukumu.
6. Boresha miundombinu ya mahakama za chini, mwanzo na wilaya ambapo wananchi wengi wanategemea huduma huko kuliko mahaka kuu n.k.
7. Ukiwa mpole tu wajanja watakuchezea watatumia udhaifu huo kukuzidi kete na kufanya maamuzi kwa niaba yako au kukuburuza. Kamwe usiwe mpole, kuwa makini na mkali kwenye mambo ya msingi, fuatilia mambo kwa karibu vinginevyo utadanganywa.