DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Mcheche Masaju, amesema kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza sheria katika maeneo ya Mahakama, akibainisha kuwa hakuna mahakama inakosa ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Jaji Masaju ameeleza hayo Septemba 29, 2025 alipokuwa akihitimisha mkutano kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki Mahakamani katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
"Hii ni pamoja na kwamba Jeshi la Polisi litaendelea ‘ku-inforce law and order’ mahakamani, Mahakama ya wapi ambayo inakosa ulinzi? Na katika kipindi ambacho akili za watu zimeharibika kiasi hiki? Watu wanazungumzia mambo, hawana tena heshima kwa viongozi wa taifa wala binadamu wenzao" amesema Jaji Masaju.
Amesema Mahakama haitaweza kukubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria mbele ya mahakama, ikiwa ni pamoja na kukemea yoyote atakayetumia mwamvuli wa uwakili kufanya vitendo visivyokubalika mahakamani.