Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma: DPP ni chujio la kwanza la haki

Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma: DPP ni chujio la kwanza la haki

Biswalo mnamuonea bure, ni nani aliweza kwenda kinyume na Jiwe kipindi cha utawala wake? Wengine si wamekimbia mpaka nchi kumuogopa Jiwe? Mlitaka Biswalo apingane naye yampate ya kumpata?
Warudishe pesa za wenyewe
Wawaachilie huru wafungwa waliobambikiziwa kesi wapinzani
Atoke hadharani aombe msamaha
Alipashwa kujitenga na uovu kwa kujiuzulu nafasi zote za uongozi
Tusiwe wadhambi
 
DPP atatenda wajibu wake lkn pia Mahakama itende haki isimwachie tu DPP akifanya ndivyo sivyo, Mahakama inawajibu wa kusimamia Haki ikitendeka na sio ikiachilia haki za Raia zikiminywa.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika kazi yake anatakiwa kuwa na nia ya kutenda Haki akimtaja chujio la kwanza katika masuala ya Haki.

Pia amesema DPP amepewa wajibu wa kuzuia matumizi mabaya ya taratibu katika mfumo wa utoaji Haki na kuangalia maslahi ya Taifa akiongeza, "Hawezi kuingiliwa na mtu yeyote, hata Jaji Mkuu hana mamlaka ya kuingilia katika kazi yake".

Aidha kwa upande wa maslahi ya Umma, Prof. Juma amesema Mkurugenzi wa Mashtaka lazima asikilize wanacholalamika wananchi na maeneo yenye tatizo.

Meanwhile National Prosecution agency is the most politicized and corrupt institution in our criminal justice system. CJ’s remarks are as good as crocodile tears. He knows the discourse very well, can’t stand a chance to unfold status quo! Maneno. Maneno. Maneno.
 
Warudishe pesa za wenyewe
Wawaachilie huru wafungwa waliobambikiziwa kesi wapinzani
Atoke hadharani aombe msamaha
Alipashwa kujitenga na uovu kwa kujiuzulu nafasi zote za uongozi
Tusiwe wadhambi
Ujiuzulu kwenye utawala wa jiwe mzee? Unajitaka? Kifupi jiwe kanyanyasa sana wateule wake, alishasema mwenyewe alikuwa anawaita wapumbavu akina Kabudi na Mpango japokuwa wamemzidi umri, sasa kama Kabudi alikuwa anaitwa mpumbavu, what about akina Biswalo?
 
Kwenye Mamlaka hizo Mama weka Waislamu wenye hofu ya MUNGU hao kina Sabaya mpaka wajirekebishe , MTU anamtaja MUNGU mara 100 Kwa siku matendo yake Hadi Shetani haamini.
 
DPP amepewa nguvu kubwa sanaaa.......na katiba sio kosa lake maana anamsikiliza No 1 zaidi anatakaje...hawezi kumbishia
... ni kosa; anatakiwa kuisikiliza katiba na sheria sio #1.
 
Katiba mpya ndio solution hapa.....hao eatendaji wa katiba
Hata ikiwepo Katiba nzuri namna gani anaweza kuja mtu akaivunja anavyotaka. Na kama watendaji wakuu wataogopa kutofautiana nae itakuwa kama toilet paper. Tunahitaji kuwa na taasisi imara ambazo ziko tayari kusimamia haki.

Marekani wasimamizi wa uchaguzi waliokuwa Republicans walikataa kabisa kupindisha matokeo kwa ajili yake. Na majaji ( ambao wengine ni Republicans) walisimamia haki na kutosa madai ya Trump. Juzi tuu Liz Cheney kavuliwa uongozi kwenye chama chake kwa kukataa kumwabudu Trump. Yote haya ni kwa sababu wana institutions imara na viongozi wanaotambua kuwa waliapa kuilinda katiba na sio mtu.

Amandla...
 
Kwenye Mamlaka hizo Mama weka Waislamu wenye hofu ya MUNGU hao kina Sabaya mpaka wajirekebishe , MTU anamtaja MUNGU mara 100 Kwa siku matendo yake Hadi Shetani haamini.
Wamisheni hawawezi kuwa na hofu ya Mungu?

Amandla...
 
Jaji Mkuu anataka kujikosha. Kuna Jaji alimuachia Lema pamoja na DPP kutaka aendelee kukaa ndani. Wakati wa kumuachia Jaji akamwambia DPP kuwa wananajis katiba ( kama sikosei). Hakimu anaweza kumpa DPP muda wa kukamilisha uchunguzi ama sivyo anaifuta kesi. Huo uwezo wanao.

Amandla...
 
Tumeanza kuwa nchi ya kutetea MAJIZI na WAHALIFU.

Kwamba kwa sasa katika nchi yetu, DPP ndiye mwenye makosa na sio MAJIZI na MAUZA NGADA.

DPP anapoyashughulikia MAJIZI na MAUZA NGADA, anaambiwa "anabambikiza".

What is "kubambikiza" in a real contextual and legal meaning?

Naona bado una hangover ya siasa chafu za yule dhalimu. Amka mzee utachafua godoro maana kumekucha. Sasa hivi lile kundi lenu la watu msiojulikana limeparaganyika, zile propaganda za kipuuzi zilizoandamana na kupika data nazo zimepita. Hivyo nakushauri utafute kazi halali, maana udhalimu mwisho ni hapo chattle ukiwa kwenye ulinzi wa kaburi la ibilisi.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika kazi yake anatakiwa kuwa na nia ya kutenda Haki akimtaja chujio la kwanza katika masuala ya Haki.

Pia amesema DPP amepewa wajibu wa kuzuia matumizi mabaya ya taratibu katika mfumo wa utoaji Haki na kuangalia maslahi ya Taifa akiongeza, "Hawezi kuingiliwa na mtu yeyote, hata Jaji Mkuu hana mamlaka ya kuingilia katika kazi yake".

Aidha kwa upande wa maslahi ya Umma, Prof. Juma amesema Mkurugenzi wa Mashtaka lazima asikilize wanacholalamika wananchi na maeneo yenye tatizo.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika kazi yake anatakiwa kuwa na nia ya kutenda Haki akimtaja chujio la kwanza katika masuala ya Haki... !!!

Biswalo plz get informed!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ikiwepo Katiba nzuri namna gani anaweza kuja mtu akaivunja anavyotaka. Na kama watendaji wakuu wataogopa kutofautiana nae itakuwa kama toilet paper. Tunahitaji kuwa na taasisi imara ambazo ziko tayari kusimamia haki.

Marekani wasimamizi wa uchaguzi waliokuwa Republicans walikataa kabisa kupindisha matokeo kwa ajili yake. Na majaji ( ambao wengine ni Republicans) walisimamia haki na kutosa madai ya Trump. Juzi tuu Liz Cheney kavuliwa uongozi kwenye chama chake kwa kukataa kumwabudu Trump. Yote haya ni kwa sababu wana institutions imara na viongozi wanaotambua kuwa waliapa kuilinda katiba na sio mtu.

Amandla...
Mkuu hapa naona umejichanganya. Umesema sahihi kwamba tunahitaji kuwa na taasisi imara. Lakini umesahau kuwa ukiwa na Katiba isiyoruhusu kuwa na Taasisi huru, Taasisi haziwezi kuwa imara. Kama kila kiongozi wa Taasisi anachaguliwa na #1 na kufutwa kazi mara moja na huyo huyo #1 anapojisikia, sahau maana huwezi jenga taasisi imara kwenye matope na kinyesi!
 
Tumeanza kuwa nchi ya kutetea MAJIZI na WAHALIFU.

Kwamba kwa sasa katika nchi yetu, DPP ndiye mwenye makosa na sio MAJIZI na MAUZA NGADA.

DPP anapoyashughulikia MAJIZI na MAUZA NGADA, anaambiwa "anabambikiza".

What is "kubambikiza" in a real contextual and legal meaning?
Mataga a.k.a sukuma gang.

Yani hamtaki kuamini kwamba meko hayupo duniani.
 
Back
Top Bottom