Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema vyama 18 vya Siasa vimeshiriki katika Mkutano wa Vyama vya Siasa, akibainisha kuwa kuna chama kimoja ambacho hakijashiriki kwa sababu bado “kinajitafuta”. Akizungumza Oktoba 7, 2026 katika mkutano huo, Jaji Mtungi amesema kila chama kina ratiba na shughuli zake za kisiasa, hivyo kutokuwepo kwa chama hicho hakuwezi kutafsiriwa vinginevyo, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano baada ya uongozi mpya kupatikana.
Soma pia >>> Rais Samia: Tuko vizuri kisiasa lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari, Tunaendelea kupokea matakwa yake
Amesema ingawa uchaguzi huambatana na ushindani na misuguano ya hapa na pale, matokeo yake huzaa washindi na walioshindwa, lakini uchaguzi unapokamilika vyama vinapaswa kurejea kuwa kitu kimoja na kujenga ari ya ushirikiano pamoja na mshikamano wa kitaifa.