Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi Mkuu ngazi ya Kata wametakiwa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, bila kupokea au kutekeleza maagizo kutoka nje ya Tume hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 5, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, wakati wa ziara yake katika mafunzo ya wasimamizi hao yanayofanyika katika Halmashauri za Mji wa Mbeya, Mbeya Vijijini (Mkoa wa Mbeya), pamoja na Mbozi na Tunduma Mji (Mkoa wa Songwe).
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Jaji Mwambegele yupo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ziara ya kukagua mafunzo hayo ya siku tatu, yaliyoanza Agosti 4 na yanatarajiwa kukamilika Agosti 6, 2025.