Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa Tume ya kutathmini matumizi ya ardhi katika eneo la Ngorongoro mkoani Arusha, Dk Gerald Ndika, amesema mfumo wa matumizi mseto ya ardhi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro umeleta mafanikio makubwa katika sekta ya utalii.
Akizungumza leo Alhamisi, Machi 12, 2026 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, Ndika amesema eneo hilo limeendelea kuwa la kipekee duniani huku idadi ya watalii ikiongezeka kutoka 592,498 mwaka 2015 hadi kufikia 884,484, Machi 2025.
“Mapato yatokanayo na utalii pia yameongezeka kutoka Tsh. 60 bilioni mwaka 2015 hadi kufikia Sh223 bilioni, Machi 2025,” amesema. Hata hivyo, amesema ongezeko la watu ndani ya eneo hilo linaongeza shinikizo la mahitaji ya maendeleo ya jamii.
“Idadi ya watu imeongezeka kutoka takribani 8,000 mwaka 1959 hadi kufikia 100,793 mwaka 2022, na inakadiriwa kufikia 276,651 ifikapo 2050,” amesema Jaji Ndika.