Jaji Ndunguru Atoa Agizo Kesi ya Lissu Ikamilike Ndani ya Siku 14

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
Jaji Ndunguru Atoa Agizo Kesi ya Lissu Ikamilike Ndani ya Siku 14

Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeongeza siku 14 za usikilizwaji wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, huku ikizitaka pande zote kushirikiana ili shauri hilo likamilike ndani ya muda huo.

Usikilizwaji wa kesi hiyo ulianza Agosti 10, 2026, na kwa mujibu wa ratiba ya Mahakama, ulitarajiwa kukamilika Septemba 7, 2026. Hata hivyo, muda uliopangwa ulifikia mwisho huku shahidi wa nne wa upande wa utetezi akiwa bado hajakamilisha ushahidi wake wa msingi.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Dunstan Ndunguru, anayesimamia jopo la majaji watatu pamoja na Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde, alitangaza kuongezwa kwa siku 14 za usikilizwaji.

Jaji Ndunguru amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kesi hiyo inakamilika ndani ya muda huo, huku akizitaka pande zote kuweka ushirikiano katika mwenendo wa shauri.

β€œMtakumbuka kuwa kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya usikilizwaji wa kesi, leo ilikuwa ndio siku ya mwisho kusikiliza shauri hili,” alisema Jaji Ndunguru.

Aliongeza kuwa shauri hilo limeongezwa siku 14 kuanzia Septemba 7, kwa lengo la kuhakikisha linamalizika ndani ya muda huo.

Jaji huyo pia amezitaka pande zote kuepuka kuuliza maswali au kuibua mambo ambayo hayana msingi katika shauri na ambayo hayatahusika katika uamuzi wa kesi, akisema kufanya hivyo kunaweza kupoteza muda wa Mahakama.

Katika hatua nyingine ya mwenendo wa kesi hiyo, shahidi wa nne wa upande wa utetezi, Brenda Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, ameendelea kutoa ushahidi kuhusu mkutano wa chama uliofanyika Aprili 3, 2025. Rupia amedai kuwa Lissu hakuwa mratibu wa mkutano huo wala hakualika vyombo vya habari.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 8, 2026, ambapo shahidi huyo anatarajiwa kuendelea na ushahidi wake wa msingi kabla ya hatua zinazofuata za usikilizwaji.


MY TAKE
1. The judge is also to blame. WHY? Katika ushahidi wa Katuga, hapakuna na ushahidi wowote wa kumfanya Lisu to have a case to answer. Ndiyo tatizo la maagizo kutoka juu! had it been that the judiciary is independent, Ndunguru would have pronounced a NO CASE TO ANSWER!


2. Ni kweli kuna upuuzi mwingi ambao hauhusiani KABISA na issue ya uhaini, ni takataka wanazileta akina Katuga.
Nilisema tangu mwanzo kuwa hakuna incriminating evidence ya kumuweka Lisu kwenye uhaini. Ujinga mtupu. Tutakinukisha in all walks of life huwezi kuihusisha na uhaini!
Uasi siyo lazima uwe uhaini, unaweza kumhasi Baba yako, lakini si kusema siyo Baba au unataka kumuua, unaweza kukataa maelekezo yake ambayo unaona siyo haki. Uasi not necessarily uwe uhaini....
 
Hivi mashahidi wa lissu akimaliza heche anafuatia nani, je wale wakenya nao watakuja ?
 
ok.
 
Shida ya hii kesi ni kwamba ukimtia hatiani Lissu kwa sababu yoyote ile, adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa

Kila mtu anajua hakukuwa na nia ya kufanya UHAINI wala Ugaidi. Hadly ingekuwa β€œuchochezi”, ambapo bado ingekuwa ngumu kuprove nani alikuwa β€œanachochewa” ili afanye nini

Jaji Ndunguru na wenzie sidhani kama wanaweza kukubali kuingizwa kwenye historia ya kutenda dhambi kubwa kiasi hicho
 
Sema yote, Lia Lia au uruke uruke lakini hukumu ni ile ile: mwenyekiti ana hatia
 
Mh Samia,Majaliwa, mpango,IGP waje mahakamani haraka ili kesi iishe mapema
 
Lakini kuna suala halijaamliwa juu ya wale mashahidi akina Samuya,Mr Plan,Katelephone na viongozi wa vyombo vya usalama kama watatoa ushahidi au la.
 
Hawa majaji tayari wameshapewa ''kimemo'' kutoka juu

Wakati Katuga anacheza na 'technicalities'' Majaji hawakuzungumzia suala la muda, walimuachia tu. Hoja ilikuwa kuacha mahakama ifuate taratibu zake, isilazimishwe . Leo ni zamu ya TL eti wanataka kesi imalizwe kwa wakati

Tunahitaji ku ''reform'' Mahakama zetu tuondokane na Ndungurus waliofelisha Taifa na kutia aibu Taaluma ya haki

JokaKuu
 
Kesi imefika mwisho naturally, ndo wanatangaza kutaka iishe. Kwanini hawakutoa kauli hizi wakati jamhuri wanaomba maahirisho kadili watakavyo? Kesi imefika mwishoni ndo wanatoa matamko

Upande wa mashtaka walijiamulia watakavyo kuipeleka hii kesi, walidharau maelekezo ya mahakama kadili watakavyo
 
Kwenye hizo siku 14 ni pamoja na wale mashahidi 7 wa Lissu ambao mahakama ilitoa pendekezo kesi kuendelea kwanza ili baadaye ije itoe hitimisho?
 
Mungu amfanyie wepesi
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Tunasubiri hukumu tuone mana chochote kinaweza kutokea!
 
Shinikizo za nje zimewakaba watu, wanashindwa kupumua. Ikiendelea baada ya hizo siku, pumzi itakata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…