Jaji Samatta: Tumeshuhudia ongezeko la uvunjifu wa Haki za Binadamu hivi sasa kuliko vipindi vingine vyote

Jaji Samatta: Tumeshuhudia ongezeko la uvunjifu wa Haki za Binadamu hivi sasa kuliko vipindi vingine vyote

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Eivz7pMWkAA7UxQ.jpeg

Jaji Mkuu mstaafu Mh. Barnabas Albert Samatta ameongelea ongezeko la uvunjifu wa haki za msingi za binadamu nchini Tanzania kuliko kipindi kingine chochote.

Amesema kuwa hivi sasa imekuwa ni kawaida kuona mtu akikamatwa na vyombo vya ulinzi na kuhukumiwa kwa tuhuma zisizokuwa na hoja yoyote ya msingi. Amesema hayo katika maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya kupigania haki za binadamu LHRC. Jaji Samatta amesisitiza umuhimu mkubwa wa taasisi hiyo kuendelea kufanya kazi nchini Tanzania hasa katika kipindi hiki.

Source:
 
Afadhali anao ujasiri wa kusema. Yule Juma ni bure kabisa, amegeuza mahakama kuwa jukwaa la magufuli kuwakandamiza wananchi.
 
Magu moyo wangu ukishamkataa.
basi tu.
Nchi ishakuw ya kinafiki kuliko,
ukisimamia haki unahatarish maish yako.
aibu sana,
yaan watu wanaangalia Magu kachek ndio nao wacheke,
Magu kasem hivi nao hivyo hivyo...
shame upon
 
Mwambieni aendelee kulea wajukuu wakati wake ulishapita.
Acha upuuzi wewe.mbona kila siku mnasimama majukwaani na kumnukuu nyerere? Huyo nyerere yupo hai?? Angetaja standard gauge hapo ungekata mauno kwa kushangilia...
 
Mwambieni aendelee kulea wajukuu wakati wake ulishapita.
Kwahio wakati ukipita na macho yanaacha kuona.....

Kati yako wewe unayemkataza kusema kile anachokiona vile anavyokiona na yeye anayeongea kitu kwa mtazamo wake nani ana walakini?
 
Hao ndio walikuwa majaji sio majaji wa siku hizi wanateuliwa kisa kuna upungufu wa majaji, walikuwa wakiamua kesi hata ukate rufaa majibu ni yaleyale hayabadiriki majaji wetu wa sasa wana mengi ya kujifunza
 
[emoji23][emoji23][emoji23],kwamba wanateuliwa kisa kuna ufungufu wa majaji,ni kama walimu wa voda fasta vile
 
Back
Top Bottom