Pia ikumbukwe Jaji Rwakibalira ni Mhaya. Kabla yake, Lema alimkataa Jaji Mujulizi (Mhaya) aliyekuwa anasikiliza keshi hii. Leama alidai hana imani na Jaji Mujulizi kwa sababu alihusika katika kashfa ya EPA akiwa IMMA ADVOCATES. Ombi la Lema lilikubaliwa na ndipo akateuliwa Jaji Rwakibalira kusikiliza hii kesi. "Kainzi" kanasema, Wahaya hawa wakakubaliana wamkomeshe huyu Lema na leo amekoma.
Kainzi haka kamelazimika kuleta harufu ya ukabila kwa kulazimishwa na hali ya kukosekana kwa uhuru wa mahakama katika taifa letu. Siyo siri majaji wetu na mahakimu wanafanya kazi katika mazingira ya kushinikizwa na wanasiasa. Tunazo documents za Ma-DC na Ma RC wakiagiza mahakimu wafanye mambo fulani ya ajabu ajabu.
Sambamba na mashinikizo ya wanasiasa kupitia majaji wafawidhi, kuna tabia ya majaji na mahakimu kulindana wakidai adui yao ni mmoja. Kesi ya nyani kumpelekea ngedere ni sawa na kesi ya Mujulizi kumpelekea Rwakibarila.
Bifu la Jaji Mujulizi juu ya Chadema halina kiwango.