Jaji Warioba haonekani sherehe za kitaifa na chama, haalikwi au hapendi kuhudhuria?

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
95,871
Reaction score
116,627
Kwanini sherehe nyingi za kitaifa Jaji Warioba huwa haonekani? Je, huwa haalikwi, hapendi kuhudhuria au ameamua kuishi kama raia wa kawaida?

Wastaafu wenzake akina Lowassa, Sumaye, Pinda na wengine huwa hawakosekani kwenye sherehe za kitaifa/kichama.

 
Si CCM wala serikali wamewahi kumuzungumzia, yaani amesahaulika kabisa. Vijana wengi hawamfahamu kama aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi.
 
Alikuwepo dodoma lakini
Tena waambie kabisa kuwa alikaa karibu na David Cleopa Msuya ndani ya ukumbi wa Jakaya Kikwete siku ya kumchagua mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu mheshimiwa sana John Joseph Pombe Magufuli.
 
Yule anamtazamo tofauti,waalikaji awataki kabisa kusikia katiba ya wananchi itawalaza njaa na kutenganisha propaganda na uhalisia
 
Ameshakuwa garasa
 

Attachments

  • 2348275_IMG-20141102-WA0010.jpg
    56.6 KB · Views: 2
Kunaweza kukawa na uhusiano kati ya hicho ulichokisema na rasimu ya pili ya katiba ya warioba, lakini bado kuna maswali mbona wakina Kabudi na Polepole wanaalikwa na kusikika vya kutosha kwenye shughuli za chama na kiserikali.
 
Si CCM wala serikali wamewahi kumuzungumzia, yaani amesahaulika kabisa. Vijana wengi hawamfahamu kama aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi.
Sure ni mtu muhimu sana huyu mzee
 
Juzi alikuwepo Dodoma! Sema hakuvaa mashati yake yale! Alikula kijani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…