Jaji Warioba haonekani sherehe za kitaifa na chama, haalikwi au hapendi kuhudhuria?

Jaji Warioba haonekani sherehe za kitaifa na chama, haalikwi au hapendi kuhudhuria?

Huyu mzee ni mzalendo sana hivyo hana mda na vitu vya porojo hata hivyo unahudhuria tu lakini SIDHANI kama anapenda tunakoelekea kama nchi
 
Huyu mzee ni mzalendo sana hivyo hana mda na vitu vya porojo hata hivyo unahudhuria tu lakini SIDHANI kama anapenda tunakoelekea kama nchi
Alishasema ukiona watu wana lazimisha kiongozi aliyepo madarakani aongezewe muda ujue yeye ndiyo anawatuma
 
Amesahaulika sana huyu mzee, but juzi Dodoma alikuwepo.
 
Kwanini sherehe nyingi za kitaifa Jaji Warioba huwa haonekani? Je, huwa haalikwi, hapendi kuhudhuria au ameamua kuishi kama raia wa kawaida?

Wastaafu wenzake akina Lowassa, Sumaye, Pinda na wengine huwa hawakosekani kwenye sherehe za kitaifa/kichama.

Kila akikunbuka alivyobutuliwa makofi halafu aliyefanya hivyo akazawadiwa u-DC anaumia sana.
 
Akina Warioba, Makamba na wazee wengine wengi tu huko CCM wameanza kuelewa kuwa kwanza, muda wao umepita na pili, lile zimwi walilolikuza na kuliimarisha kwa jeuri kibao ndio limeanza kuwageukia. Ule ubatizo wa moto waliotutisha nao sasa unawaelekea wenyewe.

Muhimu kwao sasa ni kutulia na kulinda maslahi yao kwa siku zao zilizobaki na kwa watoto wao kama tunavyoona jitihada za mzee ruksa. Hizi ni enzi za kina Makonda.
 
Back
Top Bottom