Jaji Warioba: Kikosi kazi cha Profesa Mukandala kikusanye maoni ya Wananchi wa kawaida siyo Watu maarufu pekee

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jaji Warioba amekitaka Kikosi kazi cha Profesa Mukandala na Zitto Kabwe kukusanya maoni ya Wananchi wa kawaida badala ya kualika wasomi na Watu maarufu pekee.

Jaji Warioba amesema makundi ya Kikanda, Kidini, kikabila na kisiasa vikiachiwa na kuchekewa vitaligawa taifa.

Chanzo: ITV habari
 
Tusizunguke mbuyu,tuanzie kwenye Rasimu ya pili ya Tume ya Jaji Warioba
 
Kazi ya kukusanya maoni kuhusu katiba ilishafanywa na jaji Warioba.

Hicho kikosi kazi ni batili na ufujaji wa pesa za umma.

Ccm na Serikali waache kuwafanya Watanzania mazoba.
 
Mfano:-
1. Kundi la vijana waliomaliza vyuo vikuu na vya kawaida

2. Kundi la wakulima , wafugaji, wavuvi na wachimbaji wadogo
3. Wapiga debe standi
4. Mama ntilie
5. Wakinamama walioko masokoni
6. Wafanya biashara na wamachinga
7. Wamasai waliohamishwa ngorongoro
8. Walimu, madaktari, madereva, ect
9. Wanachama wa vyama vya siasa huko vijijini
10. Wastaafu wote
 
Huyu babu anafaa sn kuwa baba wa taifa
 
Na kwanini hiki kikosi kazi fake kinapokea maoni pekee ya watu wa Dar?
 
Huyo akiongea unaweza dhani mtu,anamiliki kampun ya mikopo platnum credit,walimu wanaumizwa kule,huyo jamaa mla migebuka hamna kitu,proff nae wale wale
Uwe unatumia akili basi
Kwani Anawakopesha kwa lazima ,
Nampa hongera kwa kuwekeza akiba yake ili isaidie na watu wengine
 
Watake wasitake watarudisha Rasimu ya Warioba mezani.

Tuifanyie Maboresho muhimu.

Pesa yetu ilitumika kukusanya maoni, hatutokubali JASHO letu lipite Bure. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…