Warioba kaongea vizuri sana tena bila ushabiki, kawaeleza ukweli wanasiasa wote wa upinzani na chama tawala
1. Kawashangaa wanasema eti katiba siyo kipaumbele
2. Kasema ile rasimu yake ni maoni ya wananchi siyo rasimu yake
3. Kasema kuna mambo ya msingi wananchi waluraka yawemo mle kama vile tunu za taifa, maadili ya viongozi
4. Kasema kuwa katiba pendekezwa ile ya Chenge ina kipengele kinachosema eti Wazanzibar shurti wabadili katiba yao iendane na katiba hiyo ya Chenge, kasema hilo halitowezekana, maana katina ya Zanzibar kuna mambo mle hayawezi kubadilika mpaka maoni ya wazanzibar, Sasa huwezi kuwaconvince wazanzibar kubadili katiba yao ili kuendana na takwa hilo la katiba ya Chenge. Kasema hata kufanya hivyo kutamdistabilize rais Mwinyi ambaye sasa hivi anangoza nchi iliyotulia vizuri.
5. Warioba kamtaka rais Samia akutane na wapinzani wazungunze namna gani ya kuaporoach suala hili la katiba, mathalani kwa mfano kupitia hayo mazungumzo waone kama wanaibadili yote at once au gradually na timeframe ipi Yaani ilimradi mazungumzo yafanyike
6. Warioba kasema kuwa mtu anayepinga katiba mya huyo anapinga maoni ya wananchi
7. Warioba anasema suala la katiba mpya ni suala la kisheria, ipo sheria inayo-govern hilo suala.
8. Warioba pia amewapiga konzi wapinzani, wasiigeuze suala ka katiba mpya kama suala la kisiasa tu la kudai kwa nguvu mambo ya kuwawezesha kuingia madarakani kama vile tume huru ya uchaguzi huku wakiyapa kisogo mambo mengine ya wananchi ambayo waliyaona muhimu sana kipindi cha kukusanya maoni.