Akizungumza leo Septemba 7, 2026, kwenye Mkutano wa wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini uliondaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba amesema:
"Mmeanza jitihada za ukabila, na sasa hivi tunazungumza hata mambo ya maadili. Tunasema machifu wasimamie maadili, kwa hiyo mnataka tena turudi kwa maadili ya kikabila wakati tulikuwa tumejenga maadili ya taifa. Kwa hiyo tunarudisha kwa njia nyingine tunarudisha ukabila.
Tatu, kuna mpasuko wa dini kwa sasa hivi. Kuna mpasuko wa dini na mpasuko huo unaanza kutugawa. Na umeanza kuwagawa viongozi. Mpasuko wa dini.
Tatu, kuna ukanda. Ukanda umezidi. Tunaanza kujitazama kwa msingi wa ukanda.
Kuna utaifa umechipuka, Uzanzibari, Utanganyika. Tunaanza kujiona sisi ni Wazanzibari, sisi ni Watanganyikaa tunadai haki zetu. Uzanzibari bado wanadai wanataka autonomy zaidi hata kupata bendera. Watanganyika wameanza kudai tunataka serikali yetu na sisi tuendeshe mambo yetu. Utaifa unatugawa. Na tutakapozungumzia Katiba, tutafafanua baadhi ya mambo hayo.
Sasa tufanye nini? Nasema hapa tuone tulikotoka, ilikuwendaje tukapata umoja na mshikamano ni kwamba kulikuwa na misingi..."