Man, a 21 gun salute to Judge Warioba for keeping it 💯!
Wote tunajua tarehe 29 Oktoba 2025 hakuna watu milioni 32 waliojitokeza kupiga kura.
CCM mtandao waonyesha sura zao halisi kwenye ujenzi wa refinery Tanga.
CCM mtandao kwa mara nyingine tena wameonyesha nani hasa ni adui wa maendeleo ya nchi ya Tanzania baada ya kupinga mradi wa billionea Aliko Dangote wa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta takribani mapipa 650, 000 kwa siku! Kiwanda hiki kingeiingizia Tanzania mabilioni ya dolla kupitia kodi na ajira kwa watanzania.
Ikumbukwe Rais Ruto alisemwa na kusimangwa hadharani na Rais Samia kwa nini ametangaza ujenzi wa refinery Tanga wakati yeye Rais Samia hajui!
Rais Ruto aliomba msamaha kwa Rais Samia na akasema kama angejua asingetangaza kwani anatamani sana hiyo refinery ijengwe Kenya maana ni fursa kubwa ya kiuchumi.
CCM mtandao wamepinga ujenzi wa refinery hiyo kwa sababu ndio wanaojenga vituo vya mafuta kila kona kiholela na bei ya mafuta wanajipangia wanavyotaka, hivyo hicho kiwanda cha kusafisha mafuta kingewadhibiti pakubwa kuwaibia watanzania.
Ikumbukwe CCM mtandao ndio waliokuwa wanapinga ujenzi wa bwawa la umeme kwa sababu walikuwa na biashara kubwa ya kuingiza majenereta na dili zingine kama ile Richmond.
Ni CCM mtandao ndio walikuwa wanapinga na kuhujumu kwa namna zote mradi wa ujenzi wa SGR kwa sababu wao ndio wamiliki wakubwa wa malori.
Ni CCM mtandao ndio wamehujumu matumizi ya bandari kavu ya Kwala kwa sababu wao ndio wamiliki wa bandari kavu za mjini Dares salaam. Mpaka sehemu ya wazi Jangwani imegeuzwa kuwa bandari kavu ya kuhifadhia makontena.
Humphrey Polepole alionya kuwa CCM mtandao wamemkamata na kumdhibiti Rais Samia na sasa anawatumikia.
Rais Samia sasa anakataa viwanda kwa hofu ya kushughulikiwa na CCM mtandao.