Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema machafuko yaliyotokea Zanzibar mwaka 2001 yangeweza kuepukika kama Serikali ingeweka busara mbele na kuzuia matumizi ya nguvu kupita kiasi.
Jaji Warioba alisema hayo juzi mjini hapa, alipokuwa akichangia mjadala katika kongamano la uzinduzi wa Taasisi ya Maalim Seif Sharif Hamad kisiwani hapa.
Maalim Seif, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alifariki dunia Februari 17, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa Februari 18 kijijini kwake kisiwani Pemba.
Taasisi hiyo ilizinduliwa juzi na Rais Samia Suluhu Hassan na kusema itakuwa taasisi ya Watanzania na Serikali itashiriki kuiendesha.