Jaji Warioba: Machafuko yaliyotokea Zanzibar mwaka 2001 yangeweza kuepukika

Jaji Warioba: Machafuko yaliyotokea Zanzibar mwaka 2001 yangeweza kuepukika

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema machafuko yaliyotokea Zanzibar mwaka 2001 yangeweza kuepukika kama Serikali ingeweka busara mbele na kuzuia matumizi ya nguvu kupita kiasi.

Jaji Warioba alisema hayo juzi mjini hapa, alipokuwa akichangia mjadala katika kongamano la uzinduzi wa Taasisi ya Maalim Seif Sharif Hamad kisiwani hapa.

Maalim Seif, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alifariki dunia Februari 17, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa Februari 18 kijijini kwake kisiwani Pemba.

Taasisi hiyo ilizinduliwa juzi na Rais Samia Suluhu Hassan na kusema itakuwa taasisi ya Watanzania na Serikali itashiriki kuiendesha.
 
Tunajifunza kutokana na makosa. Huu ni wakati fika kwa serikali ya CCM kujifunza na kurekebisha makosa yao katika chaguzi ndoga na kuu Tanzania.

Kama kuna amani Tanzania, basi wadau wakuu wa walioileta hiyo amani ni VYAMA VYA UPINZANI. Amandla!
 
Yangeepukika kama pasingekuwepo na uroho wa madaraka toka kwa viongozi wa CCM.
 
Kuna kila sababu viongozi na watawala kujenga uvumilivu wa kukosolewa na kusahihishwa pale wananchi wao wanapojaribu kuwambia ukweli kama sehemu ya mitizamo yao badala ya kutaka kuckia mapambio ya kusifiwa tu.

Kumwaga damu isiyo na hatia, Mungu hakika atahukumu kwa haki siku ikiwadia.

Jaji warioba katoa ya moyoni wakati huu kulingana na mazingira ya tukio lililopo.
 
Tunajifunza kutokana na makosa. Huu ni wakati fika kwa serikali ya CCM kujifunza na kurekebisha makosa yao katika chaguzi ndoga na kuu Tanzania.

Kama kuna amani Tanzania, basi wadau wakuu wa walioileta hiyo amani ni VYAMA VYA UPINZANI. Amandla!
Mwalimu Nyerere Mwaka 1962 alianzisha kauli mbiu ya TANU iitwayo TUJISAHIHISHE.

Mwaka 1977 kuna tuliopitia Operation TUJISAHIHISHE ya JKT, na CCM ilitilia mkazo kauli mbiu hiyo.

Kina Warioba waitumie vizuri filosofia hiyo, ingawaje walioko madarakani huwa hawaipendi kwa kukosolewa.
 
Back
Top Bottom