Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Waziri Mkuu na Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, ameelezea kushangazwa na kuumizwa na wimbi jipya la ukamataji wa raia, wakiwemo wasomi, ambao wengine hufunguliwa mashtaka ya ugaidi mara tu wanapopata dhamana katika makosa ya awali.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na tovuti ya The Jenerali Ulimwengu Post kuhusu hali ya kisiasa nchini, Jaji Warioba amebainisha kuwa kuna mwelekeo wa mamlaka kutumia sheria za makosa yasiyo na dhamana kama nyenzo ya kutisha wananchi na kuwakosesha haki yao ya uhuru.
Soma Pia: Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga
Jaji Warioba ametoa mfano wa kesi ya hivi karibuni mkoani Dodoma inayomhusu mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Melkisedeki Kaijage ambaye awali alishtakiwa kwa kosa la uchochezi ambalo kisheria lina dhamana. Alieleza kuwa baada ya mahakama kuridhia kumpa dhamana, mashtaka yalibadilishwa ghafla na kuwa ya ugaidi