Jaji Warioba: Nashangaa kuona watu wanakamatwa na polisi, wanapelekwa mahakamani kwa shitaka ya ugaidi

Jaji Warioba: Nashangaa kuona watu wanakamatwa na polisi, wanapelekwa mahakamani kwa shitaka ya ugaidi

Mkuu una kazi ngumu sana ya kumtetea kilaza wa kizimkazi!
Huyo dead walking hawezi kuwasaidia kufika ikulu enyi nyumbu, amekwisha na tumeshampuuza tayari. Kazi mnayo nyie, mi yangu ni ndogo sana......kuyaweka wazi manyumbu tu basi😊😊😊
 
Umuhimu wa mabadiliko ya katiba unakuja katika hitaji muhimu la kutanua wigo wa uhuru wa watu

Ni muhimu katiba ikatamka kua makosa yote yawe na dhamana. Kama kuna issue ya usalama wa mshitakiwa au maslahi mapana ya jamii kwenye suala la dhamana basi mahakama ipewe mamlaka ya kuamua kua mtu atakaa mahabusu kwa muda gani wakati anasubiri mazingira sahihi ya kupewa dhamana huku akisubiri kusikiliza kesi yake

Kesi zote kua na dhamana itasaidia kuacha kuwabambikia watu kesi, kuacha kufungua kesi zisizo na mashiko na hata kuipunguzia serikali gharama za kutunza mahabusu. Kuna watu wapo mahabusu kwa miaka hadi kumi wakisubiri upelelezi ukamilike ili kesi zao ndio zianze kusikikizwa!!!

Bahati mbaya sana watu wenye nia ovu katika ofisi ya DPP wanatumia sheria za makosa yasio na dhamana kuwafungilia watu kesi ili tu wakae gerezani muda mrefu
 
Zee punga kweli hili. Anataka sifa kwa nyumbu, sio? Kuna kipindi chochote kimewahi pita wahalifu hawajakamatwa? Kipindi chake na Nyerere hawakukamata wahalifu?!!! Akwende zake huko zee lililofeli hilo.
Laana na iwe juu yako na kizazi chako chote muwe omba omba! Amen
 
Waziri Mkuu na Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, ameelezea kushangazwa na kuumizwa na wimbi jipya la ukamataji wa raia, wakiwemo wasomi, ambao wengine hufunguliwa mashtaka ya ugaidi mara tu wanapopata dhamana katika makosa ya awali.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na tovuti ya The Jenerali Ulimwengu Post kuhusu hali ya kisiasa nchini, Jaji Warioba amebainisha kuwa kuna mwelekeo wa mamlaka kutumia sheria za makosa yasiyo na dhamana kama nyenzo ya kutisha wananchi na kuwakosesha haki yao ya uhuru.

Soma Pia: Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga

Jaji Warioba ametoa mfano wa kesi ya hivi karibuni mkoani Dodoma inayomhusu mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Melkisedeki Kaijage ambaye awali alishtakiwa kwa kosa la uchochezi ambalo kisheria lina dhamana. Alieleza kuwa baada ya mahakama kuridhia kumpa dhamana, mashtaka yalibadilishwa ghafla na kuwa ya ugaidi

View attachment 3650836
The only honest person in the CCM gang.
 
mzee naye kazeeka sana.kama mtu anahamasisha maandamano haramu tumwiteje sasa? kama unataka maandamano fuata sheria za kuomba kibari cha maandamano .simpoooo
 
Mzee warioba ulikuwa mwanasheria mkuu wa Mwalimu Nyerere wawe ndiye uliemshauri Mwalimu Nyerere kumuweka kizuizini Mzee Abood Jumbe mpaka Mzee wa watu amefariki.je hiyo sheria kwanini mliipitisha? Kama sio wewe uliyemshauri kwanini hukujiuzuru kama njia ya kutokukubaliana na ukiukwaji wa haki za binaadamu? Lak8ni ukaamua kukaa kimya kama ishara ya kukubaliana na hali hiyo.Sasa leo unaonekana wewe unatetea haki ya binaadamu baada ya kustaafu?
 
Back
Top Bottom