Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kujadili hali ya demokrasia nchini, kufuatia matukio na hali ya kisiasa iliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, ameeleza wasiwasi wake juu ya mwelekeo wa amani na demokrasia nchini, akibainisha kuwa urejeo wa mfumo wa vyama vingi vya siasa na matumizi ya sare za vyama umezua ubaguzi mpya na kuwagawa Watanzania.
Akiangazia historia ya nchi, Jaji Warioba ameeleza kuwa kati ya mwaka 1962 na 1992, Tanzania ilikuwa na amani ya kweli na ya asili ambapo wananchi hawakuwa na hofu wala haja ya kujadili suala la amani kwani lilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Hata hivyo, amebainisha kuwa mambo yalianza kubadilika baada ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.
Ameongeza kuwa vyama vya siasa vimegeuka kuwa kama "makabila" mapya ambayo yamefanikiwa kuwatenganisha wananchi katika ngazi ya jamii na kukiuka misingi ya umoja wa kitaifa.
Akishutumu utaratibu wa sasa wa mikutano ya hadhara, Warioba ameeleza kuwa tofauti na zamani ambapo viongozi walizungumza na Watanzania wote bila kujali tofauti zao, siku hizi mikutano imekuwa ni ya wanachama pekee huku ikitawaliwa na sare zinazotenganisha wananchi.
"Siku hizi viongozi wa kisiasa wanaita mikutano ya hadhara ya wanachama yao. Chama cha siasa kikiwa na mkutano, mfano CCM inakuwa na mkutano, wanasare yao watakwenda na kijani. Ukionekana kijani pale, wa vyama vingine hawasogei pale.
CHADEMA wanasare yao, wakienda kufanya mkutano wakionekana wa kijani pale ni ugomvi. Kwa hiyo tumegawa nchi, katika siasa hata katika jamii tumegawa nchi. Ndio mwanzo ambao umetuletea matatizo katika amani yetu."-Amesema Jaji Warioba