Jaji Werema ampongeza Lissu akubali ni kifua kipana

Jaji Werema ampongeza Lissu akubali ni kifua kipana

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amempongeza Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, kwa kile alichokiita kuwa ni kuwa na kifua kipana cha kujali masilahi ya Taifa.

Jaji Werema alimwaga sifa hizo jana muda mfupi baada ya kupitishwa kwa Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalumu la Katiba.

Mwanasheria huyo anaungana na wabunge wengine akiwamo Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro (CCM), ambaye mwishoni mwa wiki alikaririwa akitaka Lissu apewe nafasi ya Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu ni mahiri katika kusimamia utaifa.

Lissu alikuwa miongoni mwa wajumbe waliopitia na kuzichambua kanuni hizo ambazo kwa sehemu kubwa, zilizua migogoro mikubwa wakati zikijadiliwa kabla ya kupitishwa.

“Tufanye kazi ya kukubaliana na kutunga Katiba yetu, tuache ushabiki wa vyama katika mambo ya msingi kama haya, lakini nawataka wajumbe waangalie mfano wa Tundu Lissu, si kawaida yake kufanya mambo ya hekima kama aliyoyafanya lakini amegeuka na kuwa ngome imara ya maridhiano ya kuzitengeneza Kanuni,” alisema Jaji Werema.

Alisema utaifa na uzalendo ndivyo vilivyomsukuma kufanya kazi hiyo bila ya kuangalia upande mmoja wa chama chake.

Akizungumzia misingi ya Kanuni, aliwataka wajumbe kuvumiliana, kuheshimiana na kupeana nafasi wakati wa kuchangia mijadala.

“Mambo ninayowaomba wajumbe kuyazingatia ni uvumilivu, werevu, kuacha mambo ya vyama, kusoma alama za nyakati na kutokuhamaki wakati wa kuchangia,” alisisitiza.
 
Alianza Ole Sendeka na sasa amefuatia Werema ngoja tumsubiri na Lukuvi naye!
 
Lissu anatumiwa na CCM kama ZZK,

Kama mnakumbuka ZZK alianza kutumiwa na Serikali ya CCM kipindi alipochaguliwa kwenye tume ya nishati ya madini, na amekuwa akitumiwa since then.

Hapa TL ametumiwa kwenye kamati ya kutunga kanuni za bunge la katiba, sasa kila mtu wa CCM anamsifia baada ya kutumiwa, TL anatumiwa na CCM, afukuzwe tu kama ZZK

Hahaha, haya CDM fukuzeni na huyu....hahahahaha!!!!!!
 
"Tufanye kazi ya kukubaliana na kutunga Katiba yetu, tuache ushabiki wa vyama katika mambo ya msingi kama haya, lakini nawataka wajumbe waangalie mfano wa Tundu Lissu, si kawaida yake kufanya mambo ya hekima kama aliyoyafanya lakini amegeuka na kuwa ngome imara ya maridhiano ya kuzitengeneza Kanuni," alisema Jaji Werema.

Hili mbona kama ni dongo, yaani Werema anag'ata na kupuliza
 
Acha uzandiki wewe...

Lissu anatumiwa na CCM kama ZZK,

Kama mnakumbuka ZZK alianza kutumiwa na Serikali ya CCM kipindi alipochaguliwa kwenye tume ya nishati ya madini, na amekuwa akitumiwa since then.

Hapa TL ametumiwa kwenye kamati ya kutunga kanuni za bunge la katiba, sasa kila mtu wa CCM anamsifia baada ya kutumiwa, TL anatumiwa na CCM, afukuzwe tu kama ZZK

Hahaha, haya CDM fukuzeni na huyu....hahahahaha!!!!!!
 
Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa TL kugombea uwenyekiti CDM.
 
Lissu anatumiwa na CCM kama ZZK,

Kama mnakumbuka ZZK alianza kutumiwa na Serikali ya CCM kipindi alipochaguliwa kwenye tume ya nishati ya madini, na amekuwa akitumiwa since then.

Hapa TL ametumiwa kwenye kamati ya kutunga kanuni za bunge la katiba, sasa kila mtu wa CCM anamsifia baada ya kutumiwa, TL anatumiwa na CCM, afukuzwe tu kama ZZK

Hahaha, haya CDM fukuzeni na huyu....hahahahaha!!!!!!

umevurugwa wewe,unadhani TL ni mchumia tumbo kama huyo msaliti wa mwandiga????
 
Jitahid kutofaitisha mambo, hata km una pumba kunako ubong jaribu kuutumia vzr, cvyo kila kitu kinafanana! Hiwezi sema Lissu anatumiwa na ccm km zzk, c bure umevurugwa!
 
Lissu anatumiwa na CCM kama ZZK,

Kama mnakumbuka ZZK alianza kutumiwa na Serikali ya CCM kipindi alipochaguliwa kwenye tume ya nishati ya madini, na amekuwa akitumiwa since then.

Hapa TL ametumiwa kwenye kamati ya kutunga kanuni za bunge la katiba, sasa kila mtu wa CCM anamsifia baada ya kutumiwa, TL anatumiwa na CCM, afukuzwe tu kama ZZK

Hahaha, haya CDM fukuzeni na huyu....hahahahaha!!!!!!

nice joke.....mh!
 
Tatizo wengi hawamielewi Lissu but for me Lissu ni mzalendo, mtu makini asiye na papara! Kinachotokea bungeni mpaka kuonekana na wa tu kwamba ni mkorofi ni kutokana na spika na wenyeviti wengi kuendesha bunge kiccm basal a ya maslahi ya nchi! Hali hiyo inaleta hasira xana, spika km makinda na kk yake ndugai ni mizigo inayoweza kukuletea hasira!
 
sasa LISU ameachana na mawazo POTOFU ya wale wakandamizaji wa CDM sasa anafuata ukweli.heko LISSU.
 
ndugu Kibo10 na wengine, ukitaka kujua wapo watanzania wengi ambao si ccm ambao ukweli hasa taifa ni muhimu kwao kuliko itikadi, tizama tu kwa uangalifu utakuta wapo wengi. fuatilia matamshi ya prof. baregu, fika kyela kaulize ni upi msimamo wa chadema kuhusu mwakyembe. chadema kuna watu wengi objective kuliko idadi ya watu objective ccm. na tatizo ni kwamba wengi katika wanaccm wanatetea maslahi binafsi wakati upande wa pili watu wanatetea maslahi mapana ya taifa.
 
sasa LISU ameachana na mawazo POTOFU ya wale wakandamizaji wa CDM sasa anafuata ukweli.heko LISSU.

Nasikia Kamati Kuu wanapanga mpango wa kujadili uanachama wake kwa kuwa amesahau kuwakilisha maslahi ya Chama na ameungana na Ole Sendeka, PM, na Werema ambao hawa wote ni CCCM, huyu ni msaliti......CDM fukuza msaliti huyu
 
sasa LISU ameachana na mawazo POTOFU ya wale wakandamizaji wa CDM sasa anafuata ukweli.heko LISSU.

hivi jitihada ya kupandikiza chuki yawezekana kwa kutumia jf ee? mh... ngoja nione mwisho utakuwa upi!
 
lissu hata mm namkubali sana nawachukia sana ccm kwa sababu ni wanafiki na washenzi wakubwa
 
Nasikia Kamati Kuu wanapanga mpango wa kujadili uanachama wake kwa kuwa amesahau kuwakilisha maslahi ya Chama na ameungana na Ole Sendeka, PM, na Werema ambao hawa wote ni CCCM, huyu ni msaliti......CDM fukuza msaliti huyu

mh....jan jaweed wanapenda ugomvi haoooo! du.....
jan jaweed.jpg
 
Nasikia Kamati Kuu wanapanga mpango wa kujadili uanachama wake kwa kuwa amesahau kuwakilisha maslahi ya Chama na ameungana na Ole Sendeka, PM, na Werema ambao hawa wote ni CCCM, huyu ni msaliti......CDM fukuza msaliti huyu
ukimsikia Lissu tu kofuli lako linaloa! kajifute hukoooo!
 
Hii nchi kuna watu wenyewe kazi yao ni kubeza kila kitu.
 
Back
Top Bottom