Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam(UDSM) ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Mwigulu Lameck Nchemba kwa kazi anayofanya akieleza kuwa chuo hicho kinajivunia nafasi aliyonayo kwani naye ni mhitimu wa chuo hicho.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo leo Disemba 20, 2025 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa kampasi ya UDSM inayojengwa mkoani Lindi
Kikwete amesema kuwa wanajivunia utendaji kazi wa Dkt. Mwigulu ambaye kuanzia shahada yake ya kwanza mpaka shahada ya uzamivu(PHD) amezipata katika chuo hicho cha UDSM.
"sisi UDSM tunaona fahari kubwa sana kuwa nawe wewe ni miongoni mwa balozi wetu wema wa chuo chetu umeanza vizuri kanyaga twende" amesema Dkt. Kikwete