Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ametoa ushauri kwa Jamii kuwatumia Wazee kupata uzoefu na maarifa huku akiweka msisitizo wa kauli aliyowahi kuambiwa na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwamba ukitaka ‘Nchi itulie kamata Wazee’ akisema ni muhimu kuwatumia Wazee kwasababu wana maarifa ambayo wameyapata katika mapito ya maisha yao.
Akiongea usiku wa kuamkia leo October 27,2024 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha kisasa cha Wazee cha Petra Elderly Centre Jijini Dar es salaam ambacho Waziri wa Ulinzi Dkt. Tax ni Mwanzilishi mwenza, Mstaafu Kikwete amesema “Askofu Mkuu Desmund Tutu aliwahi kusisitiza umuhimu wa kutambua haki na heshima ya Wazee akasema tunapozeeka haki zetu hazibadiliki, hatupotezi ubinadamu wetu wala hatupaswi kuwa wasioonekana, nasema wasioonekana maana Tanzania kuna neno wasiojulikana, ukishakuwa Mzee unaweza kuwa hauonekani kama upo sasa Waziri Stegomena na Ndugu yake jitihada anayoifanya ni kuwafanya Wazee waonekana na amesisitiza umuhimu wa kutumiwa na kushirikishwa kama Watu wanaoweza kutoa mchango muhimu katika Jamii kutokana na uzoefu, ujuzi na maarifa waliyokusanya katika mapito yao ya maisha”
“Kuwa Mzee hakukufanyi uwe sio kitu, Wazee wana maarifa mengi, mwaka 1987 nikiwa Masasi, nilikwenda Dodoma kwenye NEC Mwalimu akawa na ziara na Mimi nikapata ujiko kwamba Jakaya twende safari hii, tumefika Tanga alikuwa na tabia Mwalimu jioni anakula chakula na Wazee, siku ile pale Ikulu Wazee wakasoma risala akasikiliza hakujibu, Wazee walipoondoka akaniambia Jakaya baki”
“Akaniambia nataka kukuambia maneno uyashike la kwanza sio kila Mzee ambaye ni Mwanachama wa CCM ni Mwasisi, yule aliyesoma risala wakati tunadai uhuru hapa Lushoto ndiye alikuwa anatupinga nimeshangaa leo anasoma risala ya Waasisi wa Chama, Chama kipi?, lakini nataka kukuambia jambo lingine hili ndio la kushika, ukitaka Nchi itulie kamata Wazee, meseji kubwa pale ukitaka Nchi itulie kamata Wazee”
#MillardAyoUOUPDATES