Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Katiba gani, mbona kila baada ya miaka kumi rais akiwa ametoka bara zamu inayofuata ni visiwani wakati haimo kwenye katiba? Mbona rais akiwa mkristo akimaliza muda wake anayefuata anauwa na jina la kiislamu?

Hakuna katiba yoyote waliyolinda sababu ni kwamba miaka ingekuwa mingi sana ya wao kutopata fursa ya kutafuna rasilimali za nchi bila kuhojiwa na mtu mwenye ujasiri
Kwani katiba imekataza kiongozi kugombea bara then visiwani?...katiba imesema raisi akiwa muislam bac anaye fata lazim awe muislam au mkilsto?
 
Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maalum cha Clouds leo aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema kuwa mchakato uliokuwa mgumu zaidi kwake ni kuzuia uhuni wa kubadili muhula wa uongozi ndani ya CCM kutoka miaka mitano kuwa saba.

Jakaya anasema mjadala ulipoletwa ulikuwa ni moto ila tayarI CCM kulikuwa na utaratibu wa miaka mitano na uamuzi huo uheshimiwe.

======

KUONGEZA MIAKA YA URAIS
Kikwete:
Kuna kipindi walianza sana mjadala wa kubadili katiba sijui iwe miaka 7, pale wazee tulishauriana tukasema hapana, huku wanapotaka kutupeleka hawa sipo.

Nchi yetu ina viwango, hapa ilipofikia heshma yake kubwa ni kuheshimu vipindi viwili vya miaka mitano, wakianza hawa na miaka 7 huko tunakokwenda siko.

Nakumbuka tulikutana wazee na siku hizi hamna haja kukutana hata kwa simu mnaunganisha, tukakubaliana hawa lazima tuwaambie vijana hawa.

Mzee amesema
 
Back
Top Bottom