The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Mwaka 2019, jamaa mmoja aliyejulikana kama Aaron Smith kutoka North Carolina alizindua Singularity, app ya kutafuta wachumba mtandaoni ila iliyobuniwa kwa kanuni moja tu, kwamba hakuna mwanaume mwingine alitakayeruhusiwa kujiunga isipokuwa yeye pekee yake. Wanawake waliojiunga na programu hiyo walikuwa waki(swipe) wasifu mbalimbali na kugundua kuwa ni picha tofauti tu za Aaron zikijirudia tena na tena.
Smith alipohojiwa na vyombo vya habari alisema alitengeneza programu hiyo kutokana na kuchoshwa na majukwaa maarufu ya uchumba kama Tinder na Bumble, akitania kwamba, “tatizo kubwa la programu nyingine ni kwamba sura yangu haionekani vya kutosha.”
Suluhisho lake lilikuwa kuondoa ushindani wote na kujifanya yeye ndiye mwanaume pekee duniani anayepatikana kwa uchumba.
Kitendo hicho kilisambaa kwa kasi mtandaoni na kusababisha vicheko pamoja na mijadala kuhusu mambo ya ajabu yanayopatikana katika utamaduni wa kisasa wa kutafuta uchumba.
Baadhi ya maoni ya watu mtandaoni yalitofautiana huku baadhi yao walimsifu kama mbunifu wa kuchekesha, huku wengine wakikiona kitendo hicho kama kitu kisicho cha kawaida au ishara ya kujikata tamaa.