Ashampoo burning
JF-Expert Member
- May 12, 2023
- 1,299
- 3,977
Usiku wa Mwisho wa Uhuru
Ni Jumapili ya baridi, tarehe 18 Februari 2001. Mzee mmoja, yuko kwenye miaka ya hamsini mwishoni, anatembea peke yake kwenye bustani tulivu nje kidogo ya Washington DC. Anaonekana kawaida tu – hana wasiwasi, hana haraka, kama mtu tu kaenda kutembea. Anasimama karibu na daraja dogo la mbao, anavuta macho nyuma kidogo, anachomeka mkono mfukoni mwa koti, anatoa mfuko mdogo wa plastiki na kuuslide chini ya daraja. Drop yake ya kawaida. Rahisi, haraka, safi. Amewahi kufanya hivyo mara nyingi.
Lakini hajui leo hafanyi peke yake. Kila upande amezungukwa – ma-FBI wako kimya, wanatazama, wanasikiliza, wanashika pumzi. Miezi mingi wamekuwa wakimsubiria. Mamia ya ma-agent wameteseka kumfuatilia. Na sasa, baada ya zaidi ya miaka 20 ya usaliti, walikuwa karibu kumaliza mchezo wa msaliti mkubwa zaidi Marekani.
Mwanzo wa Usaliti
Kurudi nyuma kidogo – mwaka 1979. Kuna polisi wa zamani wa Chicago, anaitwa Robert Hanssen. Jamaa anaingia tu ofisi moja ya biashara ya Kisovieti pale New York, ambayo kila mtu anajua ni biashara fake ya wapelelezi wa Vita Baridi/cold war. Hana plan, hana connection, hana experience. Lakini ana kitu cha kuuza – siri .Miezi mitatu tu nyuma alikuwa ameacha u-polisi akaingia FBI. Sasa anawapa GRU (wale wa kijeshi wa Kisovieti) majina ya double agents wa Kisovieti waliokuwa wakifanyia Marekani kazi. Bei? Dola elfu ishirini tu. Wale jamaa walichinjwa fasta baada ya jamaa kuuza majina yao moja kwa moja. Miongoni mwao alikuwepo Jenerali Dimmitri Pyakov – legend wa Kisovieti, na chanzo muhimu cha CIA. Yule mzee alikuwa amekuwa akitoa siri kwa miaka, hadi sera za mambo ya nje za Marekani zikawa zikiegemea kwenye maelezo yake. Lakini baada ya Hanssen kumtolea, Pyakov alikamatwa, akateswa, na kuuawa. Hiyo ilikuwa pigo kubwa sana.
Kilichoshangaza ni kwamba FBI haikuwahi hata kumshuku. Hanssen akaona, “Aisee, mimi niko invisible.” Hapo ndipo akawa hatari zaidi.
Kulea Usaliti kwa Miaka
Kwa miaka 20, Hanssen akawa mkali wa drops(kuuza siri). Hakuwahi kukutana uso kwa uso na wa-Russia. Hakupiga simu. Ni dead drops tu, barua coded, files zilizofichwa kwenye vitu vya kawaida. Alijipa majina ya utani kama Ramon au B.Alishusha project kubwa kabisa – FBI walikuwa wametumia mamilioni kuchimba handaki chini ya ubalozi wa Kisovieti pale Washington ili kuwasikiliza. Hanssen akawambia Warussia . Hapo hiyo project yote ikakufa. Wa-Sovieti wakawa wanawapa FBI uongo tu kupitia hiyo tunnel/handaki .
Muda ukasogea, Hanssen akakusanya zaidi ya dola milioni 1.4, cash, diamonds, na accounts za offshore. Lakini truth ni kwamba haikuwa juu ya pesa. Jamaa alifurahia game yenyewe – ile feeling ya kuwa mjanja kuliko kila mtu.
FBI Wanachezewa
Wakati wenzake FBI wanachunguza ma-spy, Hanssen mwenyewe ndiye alikuwa anawauzia wa-Russia. Na mbaya zaidi, aligeuza tactics zote za counter-intelligence za FBI dhidi yao. Alikuwa akiwabeza kwa notes zake coded akisema ni amateurs.Wakati FBI walihisi kuna mole(msaliti) ndani, wakamshuku Brian Kelly, CIA officer. Jamaa akateseka sana – wakamfuatilia, wakamrecord, wakamuhoji. Lakini hakuna walichopata. Kwa sababu mole wa ukweli alikuwa Robert Hanssen, pale pale ofisini.