Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Achana nayo..
Maana ukisema ujiingize kwa wataalamu utakua ushajiweka kwenye system.

We achana nao fanya mambo yako mybe wakitaka kukushambulia physically ila spiritual hawatowezq hata kidogo
 
Cha msingi hama kwanza hapo weka wapangaji,ikiisha miaka mitano utarudi,mambo ya wataalamu achana nayo
 
Nakuombew ujasiri na amani ya moyo. Maneno yanakera ya watu mtaani ila huna jinsi ishatokea. Uzuri wewe ulifuata hatua zote za kinidhamu hadi kuripoti kwao, ungekuwa mbaya wala usingefanya juhudi zote hizo. Usihudhurie msiba kupisha mengi na maisha taratibu yatakuwa kawaida tena
 
Uyo jamaa anaonekana kawapiga kuku sana watu wengi ivyo watu wamemchoka ivyo mkulungwa mmoja kaona isiwe kesi kaona amtangulize mwamba mahala pena peponi. Sema wew upepo wako umekupitia vbaya ulienda kumchana ukweli ila uyo aliyemnyoosha ardhini aliona isiwe tabu namaliza kmya kmya
 
Unajuq kuwa unaweza kufungwa ikiwa umempiga mtu na Daktari akathibitisha kuwa maumivu ya kipigo ndo yamesababishia umauti.
Ikiwa mgonjwa atakufa si chini siku 367 yaani mwaka mmoja na siku..

Anyway waendelee tu kukuogopa mkuu maana mwizi anarudisha watu nyuma kimaendeleo japo inatakiwa tuwafuate watubu na kumrudia Mungu
 
Ndugu katika imani hakuna baya lolote litakufika isipokua kwa idhini ya Allah na kinyume chake ni sahihi

Just kua mtulivu mna uyo jamaa hajakuibia ww tu ilo litapita tu binadamu tumeumbwa kusahau

La mwisho ongeza ufugaji wa kuku mtaani wanakuheshimu saivi na kamwe usiende kwa wachawi kutafuta kinga muamini Mola wako tu atakulinda
 
Capitalize on fear of fools.
Sasa kuku wako wamepata Kinga. Na mnunuzi wa kuku nae akifungasha hapo utakuwa na hadhi kubwa kijijini
 
Kikubwa ni kuwa kuanzia sasa 'mali' zako zote zitakuwa salama. Hakuna atakayethubutu kuzisogelea au kuziiba. Pole lakini kwa huo mkasa wako!
 
Mwambie uyo mama akupe kuku wako hiyo ni haki yako mengine waachie walimwengu
 
Ndugu katika Imani Kuna neno zito sana ulitamka ambalo ni "MIMI NAMUACHIA MUNGU", huenda ndio matokeo ya yote hayo.
Kama ulipanga Fanya uhame, ila kama ni kwako dah sijui nini nikushauri, ila ni vizuri ukasogea eneo hilo
 
Kama hauna ubaya na mtu relax, Mungu atakupambania, usijiingize kwenye uchawi maana utatengeneza mazingira rahisi kwa wewe kulogwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…