Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Hapa napofanya Biashara Kuna ntu aliibiwa kabati la chips Na mwizi alionekana kabisa Na watu
Akakataa Na familia yake haikujali
Yule Jamaa akasema Sawa namuachia Mungu
Jamaa (mtoto mwizi) hakuamka kesho yake
Hilo tukio Ni kama miaka 10 nyuma
Mpaka Leo hiyo stori inarithishwa vizazi Na vizazi
Aisee TUNAMUOGOPA JAMAA yupo Hadi Leo
Kwa hiyo nikushauri kama hujajenga hapo Hama
Ila kama umejenga watu watakua wanakuogopa which Ina two sides
One side hautafanyiwa ujinga ujinga
Ila another side hata Maji ya kunywa watu wataogopa kuomba
 
Asante sana mkuu, umenipa ushauri nzuri sana. Acha nivumilie yatapita tu
 
Umemuomba Mungu kakulipia dhambi ulofanyiwa mshukuru

Kingine uchawi haumpati asiehusika labda kama umehusika maana wakienda kuroga watanuia aliehusika na kifo cha ndugu yao nae kimpate kitu wewe hautakuepo

Lakini kama uliamini na kumuachia Mungu wakati ulipodhurumiwa unashindwa nini kuamini na kumuomba Mungu akukinge na hilo jambo? Kuwa na imani ndugu then umesema unaendaga msikitini huwa unafuata nini kama huna imani na Mungu
 
Asante mkuu, nitaendelea na Imani yangu kama ulivyoshauri maana kama watataka kurudisha mapigo halitanikuta
 
Heshima imeamua kukufata.....sahivi hata ukisahau kitu mahali watakibeba wakuletee 😹
 
Asante mkuu
 
Hata kama jamaa hajahusika hapo itaonekana ni yeye kumbe hamna kitu
 
Jinyamazie wala usihangaike.

Hiyo siyo sifa mbaya, ni sifa nzuri ya kutisha vibaka.

kifo hicho kitakuheshimisha sana, pia jamii itakuheshimu na kukuogopa.

Hakuna kibaka atakayekuja kukuchezea tena.

Hakuna haja ya kutumia nguvu kujisafisha kwa jambo usilolitenda, iache dunia itakusafisha kwa nguvu ya Karma.

Kama alikuwa makwapu kwapu, kuna sehemu aloenda kuiba wakamkwamisha, maana kuna watu hawataki ujinga.

Potezea wala usihangaike.
 
Ndugu katika Imani Kuna neno zito sana ulitamka ambalo ni "MIMI NAMUACHIA MUNGU", huenda ndio matokeo ya yote hayo.
Kama ulipanga Fanya uhame, ila kama ni kwako dah sijui nini nikushauri, ila ni vizuri ukasogea eneo hilo
Nimejenga kabisa na ufugaji wangu naufanyia hapa
 
Ushauri wangu jambo zuri unafanya ibada, jikinge kwa Allah kwa ubaya wowote uliokusudiwa kwako,na mtake rehma yake

Amka mida ya saa nane au tisa usiku swali hata rakaa mbili na utake rehma ya Allah

Fanya hivyo hata mara tatu kwa wiki,kumbuka hakuna mchawi atakayekudhuru pasina idhini ya Allah

Lingine ikitokea labda umeitwa huko serikali ya mtaa pamoja na hao ndugu,waambe upo tayar kuapa kwa Mungu kwamba hujafanya chochote na kama umefanya laana ya Mungu ikushukie

Pili jaman muwe makini sana kuonyesha uadui au hasira yenu hadharani,kuna mtu huenda ana ubaya na mimi,sasa anasubiri wewe ukisema utaniua basi anachukua nafasi hiyo kuniua mm na ubaya unakuja kwako

Muwe makini sana juu ya mambo haya,naamini kabisa huyo ni mwizi mzoefu kwahiyo alikuwa na maadui wengi pia
 
Aisee hiyo ni hatari na nusu, kitaa wataanza kukugwaya kama mwanga kumbe kijana swafi swala tano.

Bila shala mwizi jambo la kukuibia na kukukana waziwazi lilimkereketa nafsi yake
 
Acha uoga sisi wakristo biblia imeandikwa x365 usiogope kwahiyo kila siku iambie nafsi yako usi ogope maana Mungu yu pamoja Nami amen πŸ™
 
Pole sana jirani, hata mimi niliposikia kifo cha jamaa nikajua umemroga kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…