Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

We kuwa na amani madam haukuhusika,. Apo Sasa ni Fanya TU jitihada ya kuongeza kuku hakuna atakayekuibia. Utaumiza kichwa Bure Kwa kitu ambacho huwezi kukibadilisha
 
Kaza mkuu kazaaa usiachie wapukutike wooote...nakuomba kaza

mganga nitampataje huyo
 
Samahani sana mkuu, wana JF wamenituma nikuulize, namna ya kumpata mtaalamu wako?..🤔
 
Simama katika kweli yako. Msibani nenda wala usisite. Utakayeweza kuongea nae mweleze ukweli wako na usiogope macho ya watu. Najua ni ngumu lakini Mungu wa haki atakusimamisha kwenye haki. Jiandae kisaikolojia kurushiwa vineno neno
 
ni zaidi ya mke wa mtu,...😂😂🤣
Hata majambazi sugu, wanamuogopa kuku🤔🤔🧐😂
🤓 🤓 🤓, Kabisa mkuu, kuna jamaa alienda kuiba kuku usiku, Sasa baadala ya kuwanyonga shingo ili asipige kelele, yeye akakosea akanyonga mguu 😂😂. Wacha kuku apige makelele ya kiwango cha lami.

Mpaka leo ni R. I. P
 
Mkuu hilo eneo kwako si salama na hata kwenye mazishi ya huyo mwizi wa kuku wako usikanyage kwa sababu zifuatazo; familia ya huyo jamaa hawana amani wanahisi kinaweza kuwatokea kama kilichomtokea ndugu yao hivyo wanaweza wakafanya mpango wa kukupoteza kwa lengo la kujilinda na kulipa kisasi

Kumbuka alikuja ostadhi kuomba msamaha kwa niaba ya mwizi ukasema wewe uhusiki na matatizo yake mwisho wa siku mwizi alipoteza maisha pia huyo mama aliyenunua kuku wa wizi alikuja kwako kuomba msamaha ili awe na amani lakini amepata majibu ambayo hakutegemea kutoka kwako hivyo bado umemuacha na wasiwasi atahisi kitamtokea kilichomtokea aliyeiba kuku

Kwa vyovyote huyo mama atatafuta namna ya kukumaliza ili awe na amani maana anahisi na yeye atafuata njia aliyopita mwizi wa kuku, mkuu nakushauli kama huna nguvu za kiroho hama hilo eneo haraka iwezekanavyo la sivyo itakugharimu
 
Ninakusihi sana Kwa unyenyekevu Mkubwa kushinda Ukubwa wenyewe .


Kama umepanga tu, HAMA.

Na kama ni Mji wako mwenyewe, Sijui nikushauri nini.

Ila WATAKUUA Kwa namna yoyote inayowezekana labda MUNGU ASIMAME MBELE YAKO.


Upo kwenye Mtihan mgumu sana unaohitaj utulivu wa kimaamuzi kwakua ndio yatakayoamua Maisha yako ya kesho yaan UHAI..

Wala MTU asikuambia, Kwa Sasa wanakuogopa, hawatakuchezea tena n.k .


Ikiwezekana nenda Polisi , Tafuta Wazee wa Eneo Hilo , shirikisha viongozi wa Dini wa eneo hili,wakukutanishe na Ndugu au wanajumuia wako , NACHOMAANISHA TUMIA NAMNA YOYOTE ILE UTENGENEZE AMANI NA KUAMINIWA UPYA KWENYE JAMII HIYO.

Kuna Watu wanaweza kua ni WABAYA WAKO, wameamua kupitia kwenye Hilo au watu waloibiwa na Jamaa wamemuondoa ila hekaheka zako za kufatilia kuku ,zmekufikiaha hali.
 
Uzi ufungwe,majibu yote yako hapa nilitaka kumwambia kama hivi mtoa mada.
Hapo kilichofanyika ni kwamba kuna mtu mwingine jirani ambaye alikerekwa na kuchoka tabia ya huyo mwizi kwa hiyo akautumia huo mwanya kufanya hicho kisasi halafu akajificha nyuma akijua kwa vyovyote mtu atakayehisiwa ni wewe mtoa mada kwa sababu ulijitokeza waziwazi na kukwaruzana na huyo mwizi.
Sasa kitakachofuata kuna wachawi watakuja kukujaribu waone nguvu yako inaishia wapi kwenye mambo ya giza na kama ni mwepesi mwepesi watakudhuru.
Ili kuepuka hayo madhara kwanza inabidi uhame huo mtaa lakini haimaanishi kwamba ukihama wachawi hawatokupata la hasha wachawi wakikuhitaji wana uwezo wa kukufuata popote hata iwe Ulaya tena ndani ya dakika moja tu isipokuwa ukihama itafanya watu wakusahau na kusahau tukio kwa haraka kuliko ukiwa hapohapo ukinyooshewa vidole kila siku.
Jambo lingine kwa vile umedai wewe ni muislamu tafuta wataalamu wa dua usomewe visomo vikali vya kujilinda tena inabidi usafirie sio kwa wataalamu wa mjini watakulia tu pesa yako na kukudanganya kuwa uko na kinga kumbe hamna kitu,hapa usiwe bahili wala kuwaza gharama kwa usalama wako.
Maoni yangu ni hayo zingatia haya kumbuka kuishi na walimwengu hasahasa wa uswahilini ni kazi sana ndugu inahitaji akili za ziada.
 
Hali hii ilimkuta mzee wangu alikuwa yeye na rozari rozari na yeye. Mwaka 2001 tukaibwa ng'ombe mkubwa maksai wa kulimia alituuma sana kama familia hakuna aliyekula isipokuwa watoto wadogo. kipindi hicho tuna ng'ombe kama sabini na ushee hivi lakini huyo alituuma sana.

Baasa ya siku mbili tukimtafuta maporini kutwa nzima bila mafanikio siku3 mzee akaitwa ofisi ya kijiji.Kufika akaulizwa mzee wewe ndo makanya charo? akasema mimi ndiye. Wakamwambia ng'ombe wako kapatikana shilela watu wa huku watakuwa wanapaju hapo shilela karibu na lunguya barabara ya kwenda kahama ukiwa unatoka kakola na walio leta taarifa ni mgambo (sungusungu) wa huko baada ya kumtilia shaka mwizi na kumbana hatimae alikiri kaiba.

Mzee alienda kumchukua ng'ombe ni kweli ni yeye kumbuka alienda na sungusungu wa kijijn kwetu pia jamaa yule mwizi akapigwa viboko na kuogeshwa kwenye tope na faini ya ng'ombe wa kijiji wale. Ikawa hivyo.

Mzee akaulizwa kama ana hitaji kulipwa alipwe lakini aligoma akasema kwa sababu ng'ombe wangu kapatikana na kijiji kimefuata taratibu zake mimi yameisgha kabisa.

baada ya miezi kadhaa jama aliugua kafa...Mchawi akaambiwa ni mzee. unaambiwa siku anakata roho alikuwa anawaambia kamwiteni flani aje mzee hata hajafika kwa jamaa akakuta kashafariki.


wengine wizi wa sola panel nao walikufa wakisema hivyohivyo mwiteni mzee flani.

Baada ya hapo watu wakaanza miminika kuja kununua dawa kwa mzee wakimwambia akiwapa watampa ng'ombe au hadi ng'ombe watatu.....mzee kila akiwaambia hahusiki wala hawakuamini. tangu hapo hatujawahi ibwa tena.

Huwa nafuga kuku kule sifungii kuku na muda myingine wanalala nje lakini hutasikia wameiba lakini kuna watu wanibwa vibaya mno.


2012 Walikuja wezi pia japo hawakuiba na hatukujua walikuwa wanataka waibe nini ila walikuwa wameiba na miji mingine. walipofika home hatujui kiliwatokea nini baiskeli zao wakaziacha wakaanza kukimbia ovyo sisi tumelala...bahati mbaya wanakimbilia kule walikoiba huku wanalia walikamatwa wakapigwa na kuchomwa moto

kati ya hao3 mmoja alipewa muda kwanini walikuwa wanakimbia mbio huku wanalia akasema mzee fln na vijana wake ndo walikuwa wanatukimbiza.


Mimi nilimuibia mzee 100 zile za note nafikiri mwishoni mwa miaka 90 hivi......Alinipiga vibaya mno huku akisema unataka ufe? Sijui siri ya mzee kuhusu haya ila ni mtu wa dini na nusu hata hivyo angekuwa na dawa basi mimi angekuwa kashanipa au kunielekeza.(Nipo karibu nae mno)


Mara kdhaa huwa ansema kigoma huwa hawaibwi na yeye amewahi ishi kule miaka ya 60-70 kama .....
 
Asante mkuu, nitaendelea na Imani yangu kama ulivyoshauri maana kama watataka kurudisha mapigo halitanikuta
Mkuu usidanganyike ukizubaa kitakukuta kitu.
Wachawi hawanaga hiyo akili ya kuanza kuthibitisha kwamba kweli umehusika au hujahusika.
Kwa vile wameshakushuku wewe hawapotezi muda wao wanachukua tu majina yako wanaenda kuyafanyia kazi.
Kwa hiyo kutokuwa na hatia kwako haiwezi kuwa kinga ila ni lazima upambane kujikinga,Mungu alikupa akili ili ujipambanie usikae kinyonge na kumbuka hata mwizi na mchawi wakienda kwenye shughuli zao pia wanamuomba Mungu ili wasikamatwe,kitu kingine inabidi ujue ya kuwa Mungu ni wa viumbe vyote na hana upendeleo kwa mtu mmoja kwa hapa duniani hata ufanye madhambi kiasi gani hakudhulumu haki zako hadi pale itakapofika siku ya hesabu ndipo tutahukumiwa kwa yale tuliyoyafanya duniani.
 
Kwa maelezo yako haya huyo mzee wako ni kweli kuna dawa anayo ila wewe anakuficha ila utakuja kuujua ukweli mwaka atakaofariki utaitwa ili urithishwe hiyo dawa.
Haiwezekani matukio zaidi ya mara mbili itokee hapohapo kwenu.
 
Wabongo wanawazaga mambo ya ajabu mara wawaze yesu, Allah, Muhammad, shetani,mapepo,majini,nafsi,roho,mizimu,vibwengo yaani ni vitu visivyoingia kwenye ubongo wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…